Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa Mji wa Mbalizi mkoani Mbeya kujikita katika kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo mjini Mbalizi mkoani Mbeya alipokuwa akishiriki katika ujenzi wa vyumba tisa vya Madarasa ya Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kuamsha ari ya wananchi katika kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwaunga mkono pale wanapoanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
"Wizara hii inahusika na masuala yote ya maendeleo ya kazi yetu kubwa ni kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea na kushiriki katika shughuli za maendeleo" alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano inataka kuona wananchi wanafanya kazi wanajishugulisha na shughuli za mendeleo kwa kuchangia katika miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bw. Benedict Mahenge ameishukuru Serikali wananchi na wadau walijitolea katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kwani itasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kukaa wengi katika darasa moja.
Aidha Afisa Elimu Kata ya Utengule Usingwe George Mtawa amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa umekuja kutokana na kuwa na idadi kubwa ya shule za msingi na ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba hivyo wananchi waliamua kuanza ujenzi huo ili kuondokana na changamoto ya watoto kukosa madarasa ya kusomea.
Naye Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Elia Mkono amesema kuwa wananchi wa Kata hiyo wameamua kujenga vyumba vya madarasa hayo ili kuhakikisha watoto 981 wanapata madarasa ya kuanza kidato cha kwanza katika Shuke hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa
uongozi wa Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia
vyumba tisa vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za
wananchi katika ujenzi wa madarasa hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akichanganya zege kwa ajili ya kupiga lipu katika
Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia vyumba tisa
vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za wananchi katika
ujenzi wa madarasa hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akipiga lipu katika moja ya chumba cha darasa katika
Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia vyumba tisa
vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za wananchi katika
ujenzi wa madarasa hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa Kata ya Utengule Usongwe
wakati wa zoezi la ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa katika hule hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia ramani ya jengo la mama na mtoto katika
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kitengo cha Mama na Mtoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila
mara baada ya kumtembelea ofisini kwake wakati wa ziara yake ya kikazi
mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Albert Chalamila na baadhi ya watendaji mkoa Ofisi ya rais TAMISEMI
na Wizara anayosimamia mara baada ya kuzunumza na Mkuu wa Moa huo wakati
wa ziara yake ya kikazi mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...