Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewapongeza na kuwatia moyo wale wote wanaosaidia kuboresha afya katika jamii zinazowazunguka bila kujali rika.
Mjema amesema hayo wakati wakuzindua taulo za wasichana, watoto na wazee zinazotengenezwa na kampuni ya T-Marc jijini Dar es salaam .
"Nchi yoyote ile ili isonge mbele iongeze pato la taifa ni lazima iwe na wananchi wenye afya nzuri hivyo basi taulo hizi hasa kwa wasichana zitakua mbadala wao kwani hata mahudhurio ya shuleni yataimarika hawatasita kwenda shuleni wakiwa na amani na salama kutokana na ubora na kiwango Cha taulo hizo kilivotengeneza"
Hata hivyo Mjema ameongeza kuwa watu wazima, wasichana na watoto wamekua wakipata changamoto mbalimbali za kiafya na wamejikuta wakikosa huduma hii muhimu na hivyo baadhi kuhatarisha afya zao kwa kutumia bidhaa au vitu hatarishi katika kujistiri au kuuguzwa.
Pia amewataka Kampuni hiyo waangalie uwezekano wakutengeneza kiwanda Cha taulo hizo nchini ili kuongeza kasi ya kutoa ajira kwa vijana ili kuepuka vitendo viovu vya uhalifu.
Huku Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Faustina Charles ‘Nandy’ amepata dili la kuwa balozi wa bidhaa mpya za taulo kwa watoto wadogo, wasichana na watu wazima kutoka Kampuni ya T-Marc.
Nandy amesema atashirikiana na kampuni katika kuhakikisha ulinzi wa afya za watoto, wanawake pamoja na watu wazima wenye changamoto za kiafya.
“Uzinduzi huu ni hatua muhimu sana katika kulifikia hilo na napenda kutoa pongezi kwa T-Marc nchini na wadau wake wote kwa hatua hii kubwa ya mafanikio,”
Aliongezea kuwa taulo hizo zipo kwa ajili ya wanawake Flowless, harmony kwa wazee pamoja watoto zinaitwa smiley.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waandishi wahabari katika uzinduzi wa taulo za kike, wazee pamoja na watoto kutoka Kampuni ya T-Marc nchini .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...