Na Emmanuel J. Shilatu
Sifa
kuu 3 zinambeba vilivyo Mwamba wa Afrika na jabari wa mageuzi ya
kiuchumi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli mpaka kufikia hatua Watanzania kuamua mwaka 2020 aendelee
kutuongoza.
*A: UADILIFU*
Rais
Magufuli amesimamia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo
wanaotuhumiwa kwa ufisadi Papa na ulaji rushwa wamepandishwa Mahakamani
Pia
ameimarisha uwajibikaji, uadilifu na uchapa kazi kwa Watumishi wa umma
nchini na kusimama kidete kufufua Mashirika ya umma yaliyokuwa taabani.
Mfano shirika la ndege, shirika la simu.
Halikadhalika amefanya uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya kwenye sekta ya madini.
Rais
Magufuli amedhibiti madawa ya kulevya na ujangili wa Tembo na Faru
ambapo wameongezeka kuashiria kupungua kwa biashara ya nyara za
Serikali.
Kwenye upande wa masuala ya kidiplomasia ameimarisha mahusiano mazuri na nchi jirani.
Haijawahi kutokea kwani Rais Magufuli ameweka uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za Taifa.
*B: UZALENDO*
Baada
ya Mwalimu Nyerere anayefuatia ni Rais Magufuli kutoa Elimu bure
kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari ambapo Serikali hutumia Tsh.
Bilioni 23 kila mwezi kulipia elimu bure.
Uonevu, ubabe, ubaguzi umepungua na ni sahihi kusema Rais Magufuli amepunguza uwepo wa matabaka ndani ya jamii.
Ni
wazo la Mwalimu Nyerere lakini Rais Magufuli amekuja kulitekeleza la
ujenzi wa mradi mkubwa wa Mto Rufiji wa kuzalisha umeme zaidi ya
Megawatts 2115.
Rais Magufuli amefanikiwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha na fedha kuelekezwa zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo.
Pia
Rais Magufuli yupo imara na amesimamia ukusanyaji na matumizi sahihi
ya kodi. Makusanyo yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia
Tsh. Trilioni 1.9 kwa kila mwezi.
Waliojipenyeza
kwenye ajira Serikalini bila ya sifa amewaondoa. Hivyo JPM amefanikiwa
kudhibiti vyeti feki na mishahara hewa na kubaki historia nchini.
Leo hii Watanzania tunajivunia nchi yetu, viongozi wetu, rasilimali zetu na utaifa wetu. Hivyo JPM Ameimarisha UZALENDO nchini.
Hakuishia hapo amerudisha mashamba na viwanda vilivyobinafsishwa na havikuendelezwa.
Leo
Taifa linanufaika na madini kwani amedhibiti usafirishwaji wa makinikia
na hayaendi kuchenjuliwa tena nje na madini yanauzwa hapa hapa nchini
kupitia masoko ya madini yaliyoanzisha maeneo mbalimbali yenye madini.
Huu ni uzalendo wa kuigwa wenye tija vizazi na vizazi.
*C: UCHAPA KAZI*
Leo
hii Serikali imehamia Dodoma na mpaka Rais Magufuli nae pia amehamia
Dodoma. Walisema haiwezekani lakini nia ya dhati na uchapa kazi wa Rais
Magufuli na Serikali yake imedhihirisha inawezekana.
Baada
ya reli ya Mkoloni yenye zaidi ya miaka 120, leo hii Rais Magufuli
ameanzisha Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya SGR ambayo ni reli ya
kisasa, yenye kasi na inayobeba mizigo mingi.
Sera ya Tanzania ya viwanda ipo kivitendo. Leo hii kuna ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000.
Rais
Magufuli aliapa kuilinda katiba ya nchi ambapo kuna uimarishwaji wa
amani na Uhuru wa kidemokrasia ndani ya nchi. Mathalani Umoja wa Mataifa
(UN) umempongeza Rais Magufuli kudumisha amani na usalama ndani na nje
ya nchi.
JPM amesimamia vyema ukuaji wa uchumi uliokuwa na kufikia 7.1%
Kwenye afya napo pamenoga kuna ujenzi wa vituo vya afya kila kata na ujenzi wa Zahanati kila kijiji.
Serikali ya Rais Magufuli imedhibiti maandamano ya kisiasa na ya kijamii (Mf. Wanafunzi, Madaktari) na sasa yamebaki historia.
JPM amenunua ndege mpya 8 za kisasa na Leo hii ATCL imefufuka inachanja anga za kitaifa na kimataifa.
Ameweka mikakati mizito ya kupunguza foleni kwa Ujenzi wa flyover ya Tazara na interchange ya Ubungo.
*Na Shilatu E.J*
Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...