Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipata maelezo ya Ujenzi cha Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba
ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba katika Kijiji cha Pujini Wilaya Chake
chake Mkoa wa kusini Pemba baada ya kuweka Jiwe la msingi ujenzi wa
Vituo hivyo leo tarehe 06 Januari 2020 ikiwa ni moja ya Shamrashamra za
kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020
katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Mohammed Said.

Viongozi na
Wananchi wa Pujini kisiwani Pemba wakimsikiliza Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa wakati alipokuwa
akihutubia Wananchi wa Pujini Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pemba baada
ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya
Vituo 22 vya Unguja na Pemba leo tarehe 06 Januari 2020 ikiwa ni moja ya
Shamrashamra za kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12
January 2020 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa Kusini Pemba Mhe. Hemedi Suleiman Abdalla alipowasili Uwanja wa
Ndege wa Chakechake kisiwani Pemba leo tarehe 06 Januari 2020 kwa ajili
ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya
Vituo 22 vya Unguja na Pemba katika Kijiji cha Pujini Wilaya Chake chake
Mkoa wa kusini Pemba ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa
Amani Mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia
Viongozi na Wananchi wa Pujini katika Uwanja wa Shule ya Sekondari
Pujini Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pembalepo Januari 06,2020 baada ya
kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo
22 vya Unguja na Pemba ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa
Amani Mjini Zanzibar.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...