Mhandisi wa ujenzi wa Chuo cha
Ufundi Stadi (VETA) Rukwa Ding Fubing pamoja na Mshauri Elekezi wa mradi
wa ujenzi wa Chuo hicho Swalehe Kyabega wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi
la polisi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akitaka maelezo kutoka kwa mshauri
elekezi wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa Swalehe
Kyabega juu ya maendeleo ya mradi huo na namna alivyousimamia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mhandisi wa ujenzi wa Chuo
cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa Ding Fubing pamoja na wataalamu wengine
wakalipokuwa wakitembelea mradi wa ujenzi wa chuo hicho mjini
Sumbawanga.

Baadhi ya Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa
……………….
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameagiza kukamatwa kwa
mhandisi wa ujenzi Ding Fubing pamoja na mshauri elekezi wa mradi wa
ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa Swalehe Kyabega kutokana na
kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati huku wakiendelea kusuasua
juu ya ukamilifu wa ujenzi huo ambao ulitakiwa kukamilika 30.12.2019
baada ya kuongezewa siku 100 na hatimae hadi sasa wamefikia asilimia 52
ya ujenzi.
Prof. Ndalichako
alisema kuwa kimkataba mkandarasi huyo alitakiwa kuthibitisha kwa risiti
matumizi ya shilingi bilioni 1.5 malipo ya awali ya ujenzi kupitia kwa
Mshauri elekezi ambae alishindwa kutoa vielelezo vinavyoonesha
utekelezaji wa takwa hilo la kisheria na kuongeza kuwa mshauri huyo
ameshindwa kusimamia matumizi ya fedha za serikali katika utekelezaji wa
mradi huo.
“Mkandarasi aende
akakae ndani mpaka vile vifaa mlivyoruhusu viondoke hapa, mpaka
vitakaporudi ndio muwaachie, wasababu naona sasa hii inakuwa ni
kuchezeana, majibu hamna kitu ambacho kinachoeleweka, utakwenda kukaa
sero hadi utakapotoa maelezo ya ufasaha juu ya jambo hili, kwasababu
huwezi kucheza na serikali namna hii, mara ya mwisho nilipokja hapa
mlikuwa na vifaa kama vyuma chakavu, mmeleta vifaa ahalafu mmeviondoa
kuvuipeleka sehemu nyingine, utakaa ndani hadi vifaa hivyo vitakaporudi
na uwe na watu wa kutosha kufanya kazi, kwasababu tumechoka tunataka huu
ujenzi uishe, wachukue wakae ndani,” Alisisitiza.
Halikadhalika
mhandisi huyo alionekana kuwafanyika kazi wafanyakazi wa mradi huo kwa
malipo ambayo yapo kinyume na mkataba wa serikali huku baadhi ya
watendaji wengine wa sekata ya umeme wakilalamika kufanyishwa kazi bila
ya mkataba maalum.
Prof. Ndalichako
aliyasema alipotembelea ujenzi wa chuo cha ufundi Stadi VETA katika eneo
hilo la Kashai lililopo Manispaa ya Sumbawanga huku akiongozana na
watumishi idara ya elimu kutoka halmashauri mbili za wilaya ya
Sumbawanga, Mkuu wa Wilaya hiyo, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
pamoja na uongozi wa VETA taifa.
Awali akisoma
taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho Mkurugenzi Mkuu wa VETA
nchini Dkt.Pancras Bujuru alisema kuwa mkandarasi huyo tayari amelipwa
shilingi 3,507,174,603 ambayo ni sawa na asilimi 35 ya thamani ya mradi
huo na malipo ya mwisho yalikuwa shilingi 330,521,213.79 ambapo alilipwa
tarehe 20.12.2019 na kutegemea kuwa baada ya malipo hayo kasi ya ujenzi
ingeongezeka lakini haikuwa kama walivyotaraji.
Mh. Waziri kwa
hali hii mkandarasi amethibitisha uwezo mdogo kutekeleza mradi huu na
hatuna imani kama utatekelezwa kwa wakati kwasababu muda aliopewa na
kuongezewa siku 100 vyote vimekwisha nab ado kazi hazijaweza kuisha kwa
muda, kwahiyo tunadhani kwamba uwezo wake wa kutekeleza mradi
hauturidhishi hata sisi, mshauri elekezi anajukumu la kumsimamia
mkandarasi kwa niaba yetu kwasababu tumemuajiri kwa kazi hiyo, tunajua
kwamba amekuwa akitoa maelekezo lakini kumekuwa na udhaifu wa
kuyasimamia kwa kuchukua hatua zinazostahili na kwa muda muafaka naye
tunadhani ana mapungufu,” alisema.
Tarehe 31/8/2019
mkandarasi Tender International alikabidhiwa kiwanja kwaajili ya kuanza
ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika Manispaa ya Sumbawanga
pamoja mshauri Elekezi wa Mradi huo Sky Architect Consultancy Ltd,
ambapo mradi huo ulitegemewa kukamillika mwezi Septemba 2019 huku
gharama za mradi huo ikiwa shilingi 10,700,488,940.05.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...