Charles James, Michuzi TV
ILI kuondoa changamoto ya maji nchini na kuendana na sera ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuwatua akina Mama ndoo kichwani, watumishi wa Wizara ya Maji wametakiwa kuwa wazalendo wenye kujali maslahi ya wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji nchini, Prof. Makame Mbarawa leo jijini Dodoma alipokua akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA).

Prof. Mbarawa amesema Wizara ya maji kwa muda mrefu imekua ikikabiliwa na watumishi wasio wazalendo, uadilifu wenye kuweka mbele maslahi yao binafsi badala ya wananchi maskini ambao wamekua wakikabiliwa na changamoto ya maji.

Amewaagiza wajumbe wa bodi hiyo ya 
RUWASA kuhakikisha wanasimamia vyema mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kuzuia ubadhirifu wa fedha za wananachi wanyonge ambazo zimekua zikiliwa kwa uzembe wa watu wachache.

" Uelekeo wa mwaka 2020 ni lazima ushirikiano kati ya mamlaka za maji na Ruhasa uwepo, kila mmoja awe mzalendo kwa Taifa lake kwa kusimamia rasimali zetu kwa maslahi mapana ya Nchi yetu.

Haiwezekani pamoja na ubovu wa miradi inayofanywa na wakandarasi, udanganyifu wanaotufanyia kwenye bei za manunuzi bado tunakaa kimya hatuchukui hatua. Niwatake wajumbe wa bodi hii kutumia taaluma zenu katika kuwatumikia wananchi wetu," Amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kitendo cha watendaji wa wizara hiyo kutotembelea miradi ya maji kinasababisha kwanza wizara kutojua miradi yake pamoja na kuruhusu ubadhirifu wa fedha kufanywa na wakandarasi wanaopewa miradi hiyo.

" Upo mradi tuliletewa bei za manunuzi ya vifaa ya uongo kabisa, mkandarasi alisema bei ya manunuzi ni Sh 610 Milioni lakini sisi tumefuatilia tukagundua gharama ya bei za manunuzi ni Sh 250 Milioni.

Siyo mradi huo tu miradi mingi sana wakandarasi wanataja bei za manunuzi ambazo siyo za kweli, ukienda field huko unakutana na ubadhirifu mkubwa wa fedha. Ndugu zangu tumeaminiwa na Serikali twendeni tukawatumikie wananchi wetu," Amesema Prof Mbarawa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema ni jambo la aibu endapo wakandarasi wasio na vigezo watapewa miradi ya maji ilihali Ruhasa ipo.

Amesema serikali imeanzisha 
RUWASA ili kuondoa changamoto ya maji vijijini na kuhakikisha wananchi wanachota maji bombani na kuepukana na kero ya muda mrefu ya kufuata maji umbali mrefu.

" Mmeaminiwa kila mmoja katika nafasi zenu, mnatosha na ndio maana mpo hapo, nendeni mkafanye kazi kwa ajili ya watanzania wanyonge ambao wameiamini serikali yetu. Tumieni taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa letu.

Serikali ya awamu ya tano ni ya vitendo zaidi siyo ya mchakato, hatutomvumilia yeyote ambaye tutagundua ana nia ovu kwa wananchi. Tunataka kila sehemu watu wachote maji bombani na ndio maana nyie mmeteuliwa hapa. Kafanyeni kazi," Amesema Aweso.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ruhasa, Prof Idris Mshoro ameishukuru serikali kwa ruzuku na msaada inaotoa kwa 
RUWASA ambapo anaamini kwa uwekezaji ambao unafanywa changamoto ya maji nchini inakwenda kumalizika ndani ya kipindi kifupi.

" Sisi kama bodi tunaahidi kufanya kazi kwa uzalendo tukisimamia wakala huu uadilifu, uwajibikaji na bidii kwa kuhakikisha wote wanaofanya kazi na watakaopewa kazi za maji ni wale tu wenye sifa na vigezo na siyo vinginevyo," Amesema Prof Mshoro.

 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa (kulia) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya RUWASA, Prof Idris Mshoro baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Ruhasa na watumishi wa Wizara ya Maji wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo leo jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Ruhasa, Prof .Idris Mshoro akizungumza kwenye uzinduzi wa bodi hiyo uliofanywa na Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akiwa na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijiniRUWASA leo jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa RUWASA uliofanywa na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
 Wageni mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa RUWASA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa.
 Wageni mbalimbali wakiwemo watumishi wa Wizara ya Maji waliojitokeza kwenye uzinduzi wa bodi hiyo leo.
 Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa akizungumza kwenye uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa RUWASA leo jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Patrobas Katambi na kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...