
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Singida leo na kuwasisitizakurasimisha kazi zao pamoja na kujisajili,katika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuimarisha tasnia hiyo kilichoandaliwana Bodi ya Filamu Tanzania.

Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo akizungumza na wadau wa tasnia ya Filamu Mkoa wa Singida leo kuhusu mikakati ya bodi ya filamukatika kuimarisha mazingira ya usambazaji wa kazi za filamu nje ya nchi ambapo wameipata kampuni kutoka Nigerea itakayo nunua filamu mia moja zenye hadithi zaasili ya kitanzania,wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ,wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya
Singida Wilson Shimo na wa kwanza kuliani Afisa Utamaduni Mkoa wa Sngida Bw.Hendry Kapera.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza aliyeketi watatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu Mkoani Singida leo mara baaada ya kulamizika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kueleza mipango ya serikali katika kuimarisha sekta hiyo na kuthibibiti uharamia wa kazi za filamu na kuhakikisha msanii ananufaika na kazi yake,wa pili kulia Kaimu ni
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo pamoja na Katibu TawalaWilaya ya Singida Wilson Shimo.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyeketi watatu kushoto) akitizama filamu ya masanii wa filamu Maria Luyaaliyomkabidhi wakati alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tansia ya filamu mkoa wa singida hawapo pichani,wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya FilamuTanzania Dkt.Kiagho Kilonzo, na wapili kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Singida Wilson Shimo.
***************************
Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonzaamewasisitiza wanatasnia ya filamu kuhakikisha wanarasimisha kazi zao na kujisajili.
Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hiyo leo Mkoani Singida alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kutaka kusikiliza kero zao nakuwaeleza wadau hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo,kuthibitiuharamia ili kuhakikisha wanafaidika na kazi zao.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wanatasnia hao wa filamu kuzingatia suala la uandaaji wa muswada wa filamu na kupelekamiswada hiyo kwa maafisa utamaduni kwa ajili ya ukaguzi na kupata ushauri wa filamu watakayoandaa sababu hiyo ni moja ya njia itakayosaidia kuandaa kazi zenye
ubora.
“Kwanza ningependa niwashauri muache kusambaza au kuuza kazi zenu kwa njia ya ‘flash’ katika vibanda vya kuuza filamu sababu hii bado ni njia inayowakandamiza nahauwezi kupata faida ya kazi yako, sasa hivi kazi hizo za filamu zinasambazwa kwa mfumo wa kidigitali mfano kwenye Swahilifilx na Netflix,kikubwa ni kazi yako iweyenye ubora na iliyozingatia utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa filamu ikiwemo wachezaji kuvaa uhusika na kucheza katika maeneo yenye uhalisia wa filamuhiyo,”alisema Mhe.Shonza.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo bodi imekuwa ikitoa mafunzo kwa wadau wa tasnia hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandaa kazi bora zitakazo kuwa na ushindani kwa ndani na nje ya nchi na kwa hivi karibuni wanatarajia kufanya mafunzo hayo mkoani Dodoma na kwa wadau wa Singida ambao hawajawahi kupata mafunzo hayo wanakaribishwa kushiriki.
“Bodi ya filamu katika kuimarisha masoko ya usambazaji wa filamu ndani na nje ya nchi imempata mdau kutoka Nigeria mwenye Kampuni iitwayo ENVIVO ambaye yupotayari kununua jumla kazi mia moja mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu,zenye hadithi mbalimbali za kitanzania ambapo zitatafsiriwa kwa lugha kwa lugha yaYoruba,Pijini na Igbo kusambazwa,kikubwa katika kazi hizo ni ziwe zimebeba hadithi za kitanzania na zenye ubora na pia ziwezinaendana na muswada,”alisema
Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo Dkt.Kilonzo aliwasihii wadau hao kuwa mfumo wa usambazajiwa kwa kazi za filamu kwa sasa umebadilika na filamu kwa sasa mara baada ya kukamilikainafanyiwa uzinduzi katika majumba ya sinema na huko itaonyeshwa kwa kipindi fulani na baadae inapelekwa katika mifumo mingine ya kidigitali na hatua ya kuiwekakatika CD na Youtube niyamwisho hii ni katika kulinda kazi hizo na uharamia pia kuhakikisha msanii anapata faida ya kazi yake.
Kwa upande wa Afisa Utamaduni Mkoa Bw.Hendry Kapera alisema wasanii wengi wa filamu katika mkoa huo hawataki kujisajili wala kurasimisha kazi zao hii nichangamoto kubwa na wamekuwa wakijiweka mbali na maafisa utamaduni wa wakihofia kuulizwa kuhusu usajili na hii imechangia wao kuandaa kazi zisizo na uborasababu hawapendi kushirikiana na maafisa hao.
Halikadhilika nae mmoja ya wasanii hao wa filamu kutoka Wilaya ya Ikungi Bw.Salumu Ntandu aliomba bodi ya filamu kuwapatia mafunzo wadau hao wa mkoahuo na pia aliwasihii wasanii wenzake kuwa na umoja na kuacha migogoro kwani umoja wao ndiyo utakaoweza kutangaza kazi zao na kutangaza mkoa wao palewatakapo andaa kazi nzuri zenye ubora na kushirikishana katika kuitangaza na kuizindua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...