Afisa Maendeleo
ya Jamii Kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Matias
Haule akiongea na wanafunzi wa Bai Sekondari wakati wa Kampeini ya
kupambana na VVU kwa vijana jana wilayani hapo Mkoani Dodoma.

Wanafunzi wa Bai Sekondari
wakifuatilia jambo wakati wa Kampeini ya kupambana na VVU kwa vijana
jana wilayani hapo Mkoani Dodoma.
*****************************
Serikali imetaja
vichocheo vinavyochangaia maambukizi ya VVU kwa kundi la wasichana na
wavulana kuwa ni kutokana na baadhi ya vijana kutopenda kufanya kazi
halali za kujipoatia kipato na hivyo kuendekeza biashara ya ngono kama
njia nyepesi ya kujipatia mahitaji muhimu.
Akiongea na
baadhi ya Wazee Maarufu pamoja na baadhi ya viongozi wa dini Wilayani
Bai Mkoani Dodoma jana Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bw. Matias Haule
alitaja Maudhui mabaya ya picha zisizofaa kuwa pia kichocheo cha
Maambukizi hayo.
Bw. Haule
aliitaja mitandao ya Kijamii kama vile twitter, Whats App pamoja na
Instagram kuwa inachukua muda mwingi wa vijana na muda wote unatumika
kufuatilia matendo ya ngono hivyo kuchochea maambukizi na kupelekea hata
kupata udhalilishaji wa kingono mtandaoni.
Afisa huyo
pia aliitaja mikesha na ngoma za usiku kama vile midundiko na vigodolo
kupigwa marufuku katika Jamii kwasababu sherehe hizi uwavutia vijana
wengi zaidi ambao kwa sasa wanapata maabukizi yz VVU kwa wingi kuliko
makundi mengine katika Jamii.
Aidha Bw.
Haule amutaja uelewa mdogo wa maabukizi ya VVU kwa vijana na baadhi yao
kutozingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI ikiwemo
matumizi mabaya ya kondomu ni sababu kubwa inayochangia vijana wengi kwa
sasa kutumbukia katika janga la UKIMWI.
Bw. Haule
hakuwaacha mbali wazazi na walezi kwani ameonya kuwa wazazi wanachangia
katika malezi mabovu ya vijana kwa kushindwa kutoa ulinzi kwa vijana
hasa wa kike na kuwashawishi kuijiingiza katika ngono zembe,ubakwaji na
ulawiti.
Wizara ya
Afya Maendealeo ya Jamii kwa Kushirikiana na TACAIDS pamoja na Shirika
la TASAF wako Mkoani Dodoma kutembelea wasichana barehe na wanawake
vijana pamoja na Shule mbalimbali Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha
vijana juu yatishio jipya la maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na zoezi
hili litaendelea kwa Mkoa wa Morogoro na baadae Nchi Nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...