Na Karama Kenyunko globu ya Jamii.
SHAHIDI wa 12 katika kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo tisa wa Chadema Aida Ulomi (50) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alikaa mahabusu katika kituo cha polisi Osterbay kwa siku 14, baada ya kupigwa risasi na askari polisi siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi wa marudio ya Ubunge wa Kinondoni mwaka 2018.
Shahidi Ulomi amedai hayo leo Januari 23, 2020 wakati akitoa shahidi wake katika kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
Akiongozwa na Wakili Peter Kibatala amedai kuwa yeye ni mkazi wa Kigamboni Kisiwani kata ya Vijibweni na Februari 16, 2018 alienda nyumbani kwa mama yake mdogo anayeishi Kinondoni mtaa wa Lunguya kwa ajili ya kwenda kumuona kwa kuwa alikuwa anaumwa.
Amedai alipofika kwa mama yake mdogo alikaa hadi majira ya jioni ndipo akawa anaondoka kurudi Kigamboni, na ndipo alipokuwa njiani maeneo ya Kinondoni Studio,alikutana na magari matatu ya Polisi yaliyokuwa yakitokea upande wa Magomeni huku askari polisi wenye silaha waliokuwa kwenye magari hayo walianza kushuka kwa kuruka na kuanza kupiga risasi juu.
Amedai pale kituoni walikuwa watu mbali mbali ambapo walisikika wakisema "tukimbieni jamani ni risasi za moto hizo", ndipo na yeye akajua kuwa ni risasi na alipoona watu wanakimbia nae akakimbia kuelekea kwenye jengo la CCM ambapo akiwa anakimbia kabla ajalifikia jengo hilo la CCM watu wakawa wanamwambia ameishapigwa risasi gauni, akasimama na kuona damu zikichuruzika mguuni.
Amedai alipoona vile alikaa chini pale pale na muda kidogo wakaja askari polisi wanne wanaume wakamwambia kuwa na yeye alikuwa kwenye maandamano na kisha kuanza kumpiga ndipo walipoamua kuwaita askari polisi wa kike ili wamchukue lakini kabla ya kufanya hivyo walikwenda kuwachukua watu waliokuwa wamekimbia na kuingia katika jengo la CCM, ambapo kabla ya kuondoka kuna afande mmoja ambaye nafikiria alikuwa bosi wao aliwaambia askari kuwa yameshatokea maafa hivyo waokoteni maganda yote ya risasi yaliyopo katika eneo hilo
Alidai walipomaliza kuyaokota maganda hayo askari hiyo aliwaambia maafande wambebe na kumuingiza ndani ya gari na kuongeza kuwa wakati hayo yote yanatokea kidonda chake nilikuwa kinavuja damu na hakuna huduma yoyote ya kwanza aliyopatiwa.
"Baada ya hayo mimi na watu waliochukuliwa ndani ya jengo la CCM kwa pamoja tulichukuliwa na kupelekwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Magomeni lakini hatukukaa tukapelekwa kituo cha Polisi Osterbay ," alidai.
Alidai kuwa waliofika kituoni hapo polisi zaidi ya 10 walianza kuwapiga watu hao aliyokuwa nao kwa kutumia ngumi na fimbo na kisha baadae kuwaambia waimbe nyimbo inayoitwa 'Magufuli amechukua ameweka waaa, Makonda amechukua ameweka waaa'.
"Baada ya muda kidogo kuna mbaba mmoja aliyekuwa amevalia chati la kijani ambaye alitoa karatasi iliyokuwa na listi ya majina ambayo yalianza kuitwa na yalipoisha askari mmoja alimwambia tayari watu wako wameisha akajibu ndio na kuondoka na wale watu wengine waliobaki walikuwa wanataka fedha na kuwapatia askari na kisha kuachiwa.
" Mimi niliambia kama ninahela nitoe ili niachiwe nikawaeleza kuwa sina hata shilingi na ilipofika saa 2 asubuhi mume wangu akaja akaomba kuniona na aliponiona nilivyoumia aliwaomba maafande waliokuwepo mapokezi anipeleke hospitali lakini walikataa na kusema watanipeleka wao wenyewe," alidai.
Alidai alitibiwa katika Hospitali ya kituo cha Polisi Osterbay na alikaa maabusu kwa siku 14 mpaka alipomaliza sindano alizokuwa anachomwa.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Dk Vincent Mashinji.
Washitakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...