Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Wafanyabiashara
wa soko la Samunge mkoani Arusha wameiomba halmashauri ya jiji la
Arusha kuwaboreshea miundombinu ya soko hilo ikiwemo mitaro ambayo
imekuwa ikitiririsha maji machafu hasa kipindi cha mvua.
Aidha
wamesema kuwa,wanaomba uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha
unawasaidia kutatua kero hiyo kwani wapo hatarini kukumbwa na magonjwa
ya milipuko hasa kipindi hiki Cha mvua .
Suzan
Mollel Mmoja wa Wafanyabiashara katika soko hilo,amesema kuwa kwa muda
mrefu Sasa wamekuwa wakiuza bidhaa zao katika soko hilo huku
miundombinu ikiwa sio rafiki kwa afya za walaji.
Alisema
kuwa,kipindi cha mvua soko hilo limekuwa likifurika maji machafu
katika mtaro uliopo eneo hilo ambapo maji hayo husababisha usumbufu
mkubwa kwa wafanyabiashara hao na wanunuzi kutokana na kutoa harufu kali
.
"tunaomba sana jamani
tuboreshewe mazingira ya soko hili kwa kututengenezea miundombinu hasa
mitaro ambayo imekuwa ikitiririsha maji machafu kipindi cha mvua na
kutoa harufu kali na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji."alisema Suzan.
Naye
Mfanyabiashara mwingine ,Anita Emmanuel alisema kuwa,swala la
kutengenezewa miundombinu ya soko hilo limekuwa la muda mrefu
sana,lakini limekuwa halipatiwi ufumbuzi na hivyo kuhatarisha afya za
walaji na wafanyabiashara hao kwa ujumla.
Alisema
kuwa,wanaomba kero hiyo kupatiwa ufumbuzi wa haraka hasa katika kipindi
hiki cha masika kwani ili kuwawezesha kufanya biashara zao katika
sehemu iliyo bora na salama .
Elizabeth
Mushi Mmoja wa Wafanyabiashara katika soko hilo,alisema kuwa,wanaomba
uongozi wa halmashauri hiyo kuingilia Kati swala la utengenezaji wa
miundombinu hiyo hasa ya mitaro kwani kipindi cha mvua yamekuwa
yakifunguliwa maji machafu ya chooni ambayo hutiririka kwenye bidhaa
zao na kuwazuia kufanya biashara.
Mushi
alisema kuwa,kipindi cha mvua wamekuwa wakishindwa kufanya biashara
katika soko hilo kutokana na maji machafu yanayopita kwenye mtaro huo
kwenda kwenye bidhaa zao na hivyo kuhatarisha afya za walaji.
Hata
hivyo Michuzi Globu ilipojaribu kumtafuta Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha
,hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia swala hilo.
Picha
ikionyesha mfanyabiashara Wa ndizi wakiwa wanamuuzia ndizi mteja wao
katika maeneo ya Leganga ,wilayani Arumeru (picha na Woinde Shizza,
Arusha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...