Charles James, Michuzi TV

KAMISHNA wa Sekretarieti ya Viongozi wa Maadili ya Umma, Jaji Harold Nsekela amesema viongozi wote wakubwa wa kitaifa wamewasilisha tamko la rasimali na madeni ya viongozi wa umma.

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995 fungu la 9 (1) (a)-(c) linamtaka kila kiongozi wa umma aliyetajwa katika fungu la (4) kuhakikisha anawasilisha madeni na rasimali zake katika hati rasmi.

Akizungumza na wandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dodoma, Jaji Nsekela amesema viongozi wengine waliowasilisha matamko yao ni pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu, Majaji wote na Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Amesema kwa viongozi wengine wa ngazi za kiwilaya wameshindwa kuwasilisha matamko yao kutokana na umbali uliokuepo kutoka kwenye vituo vyao vya kazi kupeleka taarifa zao zilipo ofisi za Sekretarieti ya Maadili za Kanda.

" Ni kweli katika mkutano wangu na wandishi wa habari Desemba 24 mwaka jana nililalamika kuhusu ucheleweshaji wa taarifa kutoka kwa viongozi lakini tumegundua kuna changamoto kubwa sana kutoka zilipo ofisi zao na ofisi zetu za kanda.

Tunashukuru kuona viongozi wakubwa wa kitaifa wamekua mstari wa mbele kurudisha hizi fomu, mimi mwenyewe nimepeleka taarifa zangu kwa Mhe Rais kwa sababu ndiye napaswa kuwasilisha kwake kwa mujibu wa sheria," Amesema Jaji Nsekela.

Amesema wamepata changamoto ya kupokea taarifa za watu 366 ambao wameleta matamko yao wakidhani ni viongozi ilihali sheria haiwataji kama viongozi hivyo kushauri wote wenye sifa za kuwasilisha taarifa zao wawe wanazipeleka mapema ili kuhakikisha na kukaguliwa.

" Kuna changamoto ya watu ambao mfano wanakaimu nafasi ya Kiongozi Fulani ukifika muda wa kujaza hizi taarifa na yeye anajaza akidhani ni Kiongozi kumbe bado hajawa kamilili kwa maana bado anakaimu," Amefafanua Jaji Nsekela.

Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusiana na zoezi la viongozi wa Umma kuwasilisha matamko ya taarifa zao za rasimali na madeni. Kulia ni Katibu Idara ya Usimamizi wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili Bw John Kaole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...