Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV

Matokeo ya Kidato cha Nne 2019 yaliyotangazwa mnamo tarehe 09, Januari 2019, na Baraza la Mitihani Tanzania, yameendelea kusisimu wadau mbalimbali wa Elimu kufuatia baadhi ya Wahitimu kuonesha maajabu katika ufaulu wao.

Miongoni mwa maajabu na rekodi iliyojitokeza katika matokeo hayo, ni pamoja na waliokuwa Wanafunzi sita wa Shule ya Seminari ya Katoro iliyopo Mkoani Kagera, kufaulu kwa alama nzuri sana katika matokeo ya Mtihani huo wa kuhitimu kidato cha nne mwaka jana.

Hali hiyo imeonekana kuwashangaza walio wengi kwani si jambo rahisi sana Kwa hofu ya mtihani inavyokuwa, lakini watuhumiwa hawa wameweza kufanya vizuri baada ya kuomba nafasi hiyo Kwa mamlaka zinazohusika na kesi yao, ambapo mpaka sasa upepelezi wa kesi yao haujakamilika .

Wanafunzi hao ambao mpaka sasa wapo mahabusu Kwa kushikiliwa Kwa Tuhuma za kifo cha Mwanafunzi mwenzao kilichotokea miezi kadhaa iliyopita, wametambulika Kwa majina yao na ufaulu katika mabano kuwa ni Sharifu Amri (Division II.19), Fahad Abdul-Azizi (Division II.21), Hussein Mussa (Division II.21), Sharifu Uledi (Division II.21), Abdallah Ntarambe (Division III.23), na Usama Ramadhani (Division III.25).


 Pichani ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Katoro Sheikh Faharuddin Mustapha akitoa Maelezo mafupi juu ya Watuhumia 6 waliofanya vizuri katika matokeo yao, wakati wa Mahafali ya kuhitimu kidato cha Nne 2019.
 Pichani Mkuu wa Shule Katoro Islamic Seminary Sheikh Fakharuddin Mustapha akifafanua jambo, kuhusu watuhumiwa 6, wakati alipokuwa akizungumza na Michuzi Blog Ofisini kwake.
 Pichani ni sehemu ya wahitimu kidato cha Nne Katoro Islamic Seminary 2019, wakionekana katika nyuso za huzuni Mara baada ya kisomo maalum cha Dua ya kuwaombea wenzao watuhumiwa 6, wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni Katoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...