Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Brand Chapa Gsm,Mhandisi Hersi Said akiwa na kocha mpya wa timu ya Yanga (Young Africans SC),Lucy Eymael kutoka nchini Ubelgiji,kwa pamoja wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Zanziba mara baada ya kuwasili mapema  leo asubuhi.Kampuni ya GSM ndiyo iliyofanikisha kumleta kocha huyo mpya kwa ajili ya kuInoa vyema timu ya Yanga.


HISTORIA FUPI YA KOCHA HUYO HII HAPA 

#Yangaupdates | Mfahamu Kocha Mpya Yanga Kwa Ufupi | .

✓ 26 August 2010, aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa AS Vital ya Congo .

✓ Msimu wake wa kwanza aliisaidia AS Vita kumaliza Juu ya Tp Mazembe na kuisaidia pia kushinda  Super Coupe du Congo 2011. Pia aliisaidia kuifikisha Raundi ya pili ya michuano ya CAF Champions league. Aliweka Rekodi ya mechi 23 bila ya kufungwa na baadae 2011 April alijiuzulu kufundisha timu hiyo

✓ 2011, 1 Julai alijunga na Missile ya Gabon kama kocha mkuu, na aliisaidia timu hiyo kushinda taji lao la kwanza la ligi katika historia yao, pia akaisaidia timu hiyo kufika Raundi ya 16 CAF Confederation Cup na kupoteza goli kwa penati 0-3 dhidi ya JS Kabylie baada ya Aggr ya  3-3.

Timu Nyingine alizo zifundisha Luc ni

2013 - Leopard, 2014 - Rayon Sport, 2014/15 - Js Kairouan, 2015 - Al Nasr, 2015/16 - Al Merrikh, 2016/17 - Polokwame City, 2017/18 - Free state Star, 2018/19 - Talae's El Gaish, 2019 - Black Leopard.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...