Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya
Tume Taifa ya Uchaguzi yaliyopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma
alipotembelea kujinea namna hatua hizo zinavyoendelea.Ziara hiyo
ilifanyika Januari 07, 2020

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na
Kanali Mabele ambaye ni Msimamizi mkuu wa mradi huo kutoka SUMA JKT
wakiangalia sehemu ya majengo ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi
yanayoendelea kujengwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yake katika mradi
huo.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiweka
saini katika kitabu cha wageni alipotembelea majengo hayo.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua ujenzi wa Majengo ya Ofisi
ya Tume ya Uchaguzi yaliyopo Jijini Dodoma alipotembelea kujinea namna
hatua hizo zinavyoendelea.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
*****************************
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya
Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema
ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Alikagua mradi
huo, Januari 07, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Novemba 18, 2019 alipotembelea na
kukagua mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maagizo
hayo baada ya TBA kusimamisha zoezi la ujenzi kwa ongezeko la gharama
za kutoka bilioni 13 hadi bilioni 32 na hivyo kumtaka Waziri Mhagama
kufuatilia.
Ziara ya Waziri
Mhagama imebaini maendeleo mazuri ya ujenzi na kufikia hatua ya asilimia
75 baada ya Tume hiyo kuingia mkataba SUMA JKT kuwapongeza wakandarasi
kwa hatua hiyo wanayoendelea nayo.
“Kwa kipindi
chote ambacho SUMA JKT imeendeela na kazi ya ujenzi wa jengo hili hali
inaridhisha na ni vyema kuhakikisha mnaendana na kasi inayotakiwa kwa
kuzingatia gharama zilizokubalika za bilioni 16,”Alisistiza Waziri
Mhagama
Alieleza kuwa
ujenzi wa majengo ya Serikali ni moja ya hatua za kuhakikisha zoezi la
kuhamisha watumishi Dodoma linafanikiwa kwa kuendelea kuweka miundombinu
rafiki ya ofisi zao.
“Mpaka sasa
tayari watumishi wapatao 14868 wameshahamia hapa Dodoma hivyo
tutaendelea kuandaa mazingira ikiwemo ujenzi wa ofisi hizo kwa
kuzingatia kazi ya Uratibu huo ipo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu,”alisema Mhagama
Alifafanua kuwa,
kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuhakikisha watumishi wa ofisi hiyo
wanatoa huduma vizuri kwa kuzingatia mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi
mkuu ambapo itasadia utendaji wa kazi.
Waziri Mhagama
ameendelea kueleza kuwa , miongoni mwa majukumu ya Ofisi yake ni
kuhakikisha inaratibu shughuli zote za kuhamisha watumishi wa Serikali
na kuweka mazingira mazuri ya ofisi zao ili kuendelea kuitumikia nchi
kwa weledi na kujiletea maendeleo yao kwa kutoa wa huduma bora
zinazostahili.
Kwa upande wake
mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo Mhandisi Michael Mussa
alieleza kuwa, wataendelea kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa ili
kuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia gharama zilizofikiwa kwenye
mkataba wa ujenzi huo.
“Tumefarijika kwa
ujio wa Mhe. Waziri na tunaahidi tutajenga kwa kipindi kilichopangwa
kwa kuzingatia gharama zilizopo kwenye mkataba wa ujenzi huu,”alieleza
Mhandisi Michael.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...