Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wazalishaji wa vifungashio vya plastiki aina ya tubings vinavyotumika kufungashia bidhaa kama karanga, ubuyu na barafu, vikiwa havina kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), havina lakiri (seal) wala alama (label) kama kanuni namba 3 inavyoelekeza. Vifungashio hivi sasa vinazalishwa kwa wingi kwa ukubwa mbalimbali na vimekuwa vikitumika kama mifuko ya kubebea bidhaa sokoni.
Kwa mantiki hiyo, Katika masoko yetu hali inaonyesha kuwa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku imerudi kivingine kama ‘vifungashio’.
Aidha, Kwa mujibu wa Kanuni ya Usimamizi wa Mazingira ni Marufuku Kutengeneza, Kuuza, Kusafirisha ndani na nje ya nchi, Kusambaza na Kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.
Uwepo wa vifungashio hivi sokoni unaenda kinyume na Kanuni ya 4 (b) na (c) , Kanuni hii imeanzishwa ili kulinda afya ya binadamu, wanyama na mazingira dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza,Vilevile kutoa motisha kwa ajili ya kuhamasisha uzalishaji na uingizaji nchini wa mifuko mbadala.
Aidha, ilibainika pia, vifungashio hivi vina athari za ziada kwa watoto pale wanapotafuna vifungashio hivyo na kumeza chembechembe ndogo za plastiki. Hali kadhalika, baadhi ya wafungashaji wa bidhaa wamekuwa wakipuliza vifungashio hivyo ili kupata wepesi wa kuweka bidhaa na hivyo kuhatarisha afya ya walaji kunakoweza kupelekea kuenea kwa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa.
Kanuni ya 6 inatoa ‘zuio’ la vifungashio vya plastiki kuwa vitumike pale tu itakapobainika kuwa bidhaa husika ina ulazima wa kutumia vifungashio vya plastiki, na kwa mujibu wa Kanuni ya 3 inatafsiri ulazima huo kuwa ni “kuhifadhi ubora au kuzuia uharibifu wa bidhaa ambavyo vitakuwa na lakiri au alama inayotambulisha bidhaa iliyofungashwa kabla ya kuuzwa, kusambazwa au kuingizwa sokoni”.
Kwa kutumia vifungu tajwa hapo juu, ‘vifungashio vya plastiki (plastic wrappings) kama vinavyotumika kufungashia maji na vitu vingine havina sifa na NEMC inatoa hadi tarehe Aprili 30, 2020, visionekane sokoni.
Faida za marufuku hii ni pamoja na; Kuondokana na kero ya kuzagaa kwa mifuko ya plastiki; kupungua kwa vifo vya mifugo, kupungua kwa matumizi yasiyo rasmi ya mifuko ya plastiki katika kufunikia vyakula na kuwashia moto ambayo yanasemekana kuwa kisababishi cha Saratani , ugumba, na athari nyingine za kimazingira.
Aidha, faida nyingine ni kujitokeza kwa fursa ya kutumia rasilimali zilizopo nchini zitokanazo na miti, katani, pamba na mazao mengineyo kutengeneza mifuko ya kubebea bidhaa isiyo na athari kiafya na ambayo ikiingia ardhini huoza. Hali kadhalika kuongeza mauzo kwa viwanda vyetu vya ndani vinavyozalisha malighafi ya karatasi. Viwanda hivi vimefanikiwa kutoa ajira kwa vikundi vya wajasiriamali wanaotumia malighafi za viwanda hivi kutengenezea mifuko ya karatasi. Kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika mwezi Disemba 2019, jumla ya vikundi 2761 vya utengenezaji mifuko ya karatasi vimeanzishwa nchini, ambapo 1028 (37%) viko mkoa wa Iringa na 1733 (62%) vikiwa Dar es Salaam.
Jitihada mbalimbali zimechukuliwa ili kuhakikisha sheria inatekelezwa na changamoto zinatatuliwa. Serikali imeandaa viwango na kutoa elimu kwa wadau ili watii sheria. Jitihada hizo ni pamoja na kuandaa rasimu ya viwango vya vifungashio kwa kuwashirikisha wadau, kufanya mikutano na wadau wa sekta ya uzalishaji vifungashio ili kuwaelimisha jinsi ya kutekeleza Sheria. Vilevile NEMC kwa kushirikiana na taasisi zingine za Serikali wamekuwa wakifanya ufuatiliaji na kuwachukulia hatua wote wanaokiuka sheria.
Marufuku hii itasaidia kuwabana wazalishaji wasio rasmi, itasaidia kulinda afya za watu na mazingira, itatengeneza ajira, italinda viwanda vya ndani, itarahisisha ufuatiliaji wa sheria na itawalinda wafanyabiashara waaminifu ambao wanafuata sheria.
Kwa taarifa hii, idara zote za Serikali zinazowajibika kutekeleza sheria hii, wakiwemo viongozi wote wa masoko na viongozi wa Serikali za Mitaa husika wanatakiwa kufuatilia na kuchukua hatua husika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...