Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, Mizengo Peter Pinda, wakati akiwasili kwenye mahafali ya 38 ya
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT), katika uwanja wa Ilulu mjini
Lindi Machi 12, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, Mizengo Peter Pinda, wakati akiwasili kwenye mahafali ya 38 ya
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT), katika uwanja wa Ilulu mjini
Lindi Machi 12, 2020.
Baadhi ya wahitimu wakisubiria
kutunukiwa shahada kwenye mahafali ya 38 ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (CKHT), yaliyofanyika katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi Machi
12, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiwahutubia wahitimu, kwenye mahafali ya 38 ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (CKHT), yaliyofanyika katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi Machi
12, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, Mizengo Peter Pinda, wakati akiwasili kwenye mahafali ya 38 ya
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT), katika uwanja wa Ilulu mjini
Lindi Machi 12, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU
Kassim Mjaliwa amesema wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu mbalimbali
nchini China waliozuiwa kutokana na mlipuko wa homa ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona wote wanaendelea na masomo yao kwa
njia ya mtandao.
“Tehama sasa
imefikia katika hatua nzuri kwa sababu Mhadhili mmoja anaweza
kuwafundisha wanafunzi wake wote popote walipo kwa njia ya mtandao.
Tehama imewezesha wanafunzi waliozuiwa kurudi nchini China kuendelea na
masomo wakiwa nyumbani kwao.”
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Alhamisi, Machi 12, 2020) katika mahafali ya 38 ya
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT), katika uwanja wa Ilulu mjini
Lindi. Amesema baada ya virusi vya corona kuikumba China vyuo vilifungwa
na sasa vimefunguliwa na wanafunzi wanasomo kwa njia ya mtandao.
Pia, Waziri Mkuu
amewaeleza wahitimu wa CKHT kuwa vyeti walivyotunukiwa ni tuzo halali
kwa juhudi na jitihada walizoonesha katika masomo yao, hivyo wanaporejea
kwenye jamii wahakikishe wanaipatia tuzo ya utendaji bora na ufanisi
itakayoakisi viwango vilivyoainishwa kwenye vyeti vyao.
“Nendeni
mkaidhihirishe tuzo hii ya pili katika utendaji wenu na maisha yenu ya
kila siku, iwe ni katika sekta rasmi au sekta isiyokuwa
rasmi. Hakikisheni mnaonesha tofauti katika kutafuta majibu ya maswali
mbalimbali yanayowakabili Watanzania kuhusu mustakabali mzima wa
kujiletea maendeleo.”
Waziri Mkuu
amesema amefuatilia kwa karibu maelezo ya Viongozi waliotangulia kuhusu
umuhimu na hata mafanikio ya chuo hicho ambapo amewataka watambue kwamba
Serikali inakiangalia kwa jicho la karibu sana kwa kuwa kimekaa
kimkakati zaidi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.
Amesema licha
yachangamoto mbalimbali zilizopo, Serikali imeweza kuanzisha chuo hiko
na kukiona kikiendelea kutanuka hadi nje ya mipaka ya nchi yetu. “Haya
ni mafanikio makubwa na ya kujivunia. Tunawashukuru waasisi wa Taifa
letu kwa maono haya makubwa kuhusu Tanzania.”
Waziri Mkuu
amesema Mwasisi wa Taifa letu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
aliona mbali sana wakati akianzisha mchakato wa kuanzisha Chuo hiki kwa
kusema angependa kuona taasisi inawawezesha watu wazima wengi waweze
kuendelea na elimu ya juu pasipo kuacha kazi zao. Vilevile,
aliongeza kwa kusema, “Kwa nchi maskini kama Tanzania, hakuna Taasisi
nyingine ya elimu ya juu inayoweza kuwa ya msaada zaidi kwa watu wetu”.
Waziri Mkuu
amesema ukweli wa kauli hiyo unaendelea kudhihirishwa siku hadi siku
kupitia mafanikio ya chuo hicho. “Tutake tusitake, elimu ya juu
inayoweza kusaidia watanzania wengi zaidi ni hii ya kupitia mfumo wa
Elimu Masafa na Huria.”
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa umuhimu na thamani ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na
vyuo vingine utakuwa na maana tu pale ambapo vitakuwa na mchango kwenye
maendeleo ya nchi. “Kwa miaka nenda
rudi, chuo kimehitimisha wataalamu lukuki, ambao wengi wameingia kwenye
sekta mbalimbali za utumishi na uzalishaji na kutoa mchango muhimu sana
kwenye maendeleo ya nchi yetu.”
Wakati huo
huo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa uongozi wa CKHT na Tume ya Vyuo Vikuu
nchini (TVV) wahakikishe kuwa udahili wa CKHT unatanuliwa kwa sababu
hadi sasa chuo kina kozi moja tu ya maandalizi kwa ajili ya kuwaandaa
vijana kuingia kwenye Shahada.
Waziri Mkuu
amesema katika kuongeza udahili kwenye elimu ya juu, ameshauri wawe na
kozi ama programu za maandalizi kwa wale wanaotaka kusoma stashahada na
kwa wale wa cheti pia. Amesema matokeo
ya programu hizo yataongeza ushiriki wa Watanzania wengi kwenye elimu ya
juu. “Wito wangu kwa TCU nchini kuhakikisha inasimimia na kuongoza, kwa
kushirikiana na CKHT katika uanzishwaji wa programu hizi kwa kuzingatia
viwango vya juu vya ubora wa elimu ya juu.”
Katika mahafali
hayo, jumla ya wahitimu 698 walitunikiwa vyeti wakiwemo 20 wa Shahada za
Uzamivu (PhD) na wengine 185 Shahada na Stashahada za Uzamili, wengine
344 walitunukiwa Shahada ya Kwanza, 166 walitunikiwa Stashahada na
Astashahada mbalimbali.
Mahafali hayo
yamehudhuliwa naWaziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha
Tanzania Mizengo Peter Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mwenyekiti wa
Kamati ya Ushauri ya Chuo Mkoani Lindi Godfrey W. Zambi,
Wengine ni
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Profesa Rwekaza
Mukandala, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Profesa Elifas
Tozo Bisanda na wakuu wa wilaya za mkoa wa Lindi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...