Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akilipowasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza Hukumu ya kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo nane wa Chadema iliyokuwa ianze kusomwa saa nne na nusu asubuhi hii leo Machi 10, 2020. Hukumu hiyo imeahirishwa hadi saa saba na nusu mchana leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiteta jambo na Mshauri Mkuu wa Chama cha siasa nchini Tanzania cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa kusikiliza Hukumu ya kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo nane wa Chadema iliyokuwa ianze kusomwa saa nne na nusu asubuhi hii leo Machi 10, 2020. Hukumu hiyo imeahirishwa hadi saa saba na nusu mchana leo.
Yakiwa yamebaki masaa mawili kusomwa kwa hukumu ya Vigogo wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa Chadema umeendelea kuongezeka.
Aidha Askari nao wameonekana wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Mahakama inafikia hatua hiyo baada ya miaka miwili ya kesi hiyo kufika katika Mahakama ya Kisutu na mwaka mmoja kasoro siku nne kwa Hakimu Simba kupokea jalada na kuanza kusikiliza upya kesi hadi kufikia mwisho.
Kina Mbowe wanatarajia kusomewa hukumu baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.
Awali kesi hiyo ilipoanza Machi mwaka 2018 ilikuwa inasikilizwa na aliyekuwa Hàkimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye aliyeteuliwa kuwa Jaji Machi mwaka 2019 na jalada la kesi hiyo kuhamia kwa Hakimu Simba Machi 14 mwaka 2019.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko,aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicenti Mashinji, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na Mbunge Bunda, Esther BULAYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...