Na Shukrani Kawogo,LUDEWA

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani njombe Andrea Tsere amewataka madiwani wa kata mbalimbali pamoja na wakuu wa shule kuhakikisha wanafunzi 645 wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti shuleni kuanza masomo, wanaripoti kabla ya march 31 kuanza masomo hayo.

Agizo hilo amelitoa katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika hivi karibuni wilayani humo ambao ulishirikisha madiwani, wakuu wa shule, pamoja na wadau wengine kutoka Nyanja mbalimbali.

Alisema jumla ya wanafunzi waliokuwa wanatarajiwa kuripoti ni 3008 ambapo mpaka sasa wameripoti 2363 na 645 kuto kuripoti kutokana na sababu mbalimbali ambapo moja ya sababu hizo ni wazazi kutowaandalia mahitaji ya shule.

“Wakuu wa shule za msingi wanapaswa kupitia majina ya wanafunzi waliofaulu katika shule zao na kuangalia shule ya sekondari aliyopangiwa ambapo mkuu wa sekondari hiyo ataangalia majina hayo na kuhakiki kama wanafunzi wa majina hayo wapo shuleni au la! Na endapo itabainika hawajaripoti itakuwa rahisi kuwafuatilia kwa wazazi wao” Alisema Tsere/

Aidha wakuu hao wa shule wamelipokea suala hili kwa mikono miwili na kuahidi kuwa watalifuatilia kikamilifu na kuhakikisha wanakuza kiwango cha elimu wilayani Ludewa.

Mkutano huo wa wadau wa elimu hufanyika kila mwaka ili kubaini hatua wanayopiga katika suala la elimu pamoja na mapungufu yake ambapo kilianza rasmi mwaka 2018.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...