Mtaalam wa Huduma za Kidijitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi,akimkabidhi mfano wa hundi ya 13m/- mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2020 Miller Said Kungwi, mkaazi wa Mbagala,Dar es Salaam
===== ====== ======= ======
Mkazi wa Dar es Salaam, Miller Said Kungwi amejinyakulia 13m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2020.
Promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90(miezi 3) na wateja wa Tigo walipata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslim kila siku na droo ya mwisho mshindi alikuwa anajinyakulia zawadi ya 13m/-. Promosheni hii ilishuhudia washindi 90 kila siku waliojishindia Tshs 100,000. Pia tuliwapa washindi 12 kili wiki kwa mda wa wiki 12, Tshs 1,000,000.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Kungwi alisema “Wakati napigiwa simu,nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kuenda katika mihangaiko yangu ya kibiashara, basi nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunipika zawadi hii kwani itanisaidia katika kujiajiri na kuisaidia familia yangu “alisema kwa furaha.
· Mtaalam wa Huduma za Kidijitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.
“Tunayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wetu fedha zake. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo sasa imemalizika”. alisema Ikunda.
Aliongeza kuwa, Promosheni hii pamoja na nyengine tulizoanzisha Oktoba 2018, sasa ni msimu wa tano, na kwa jumla tumekuwa na washindi 1,904, na kwa ujumla Tigo imetoa 197,500,000/- fedha taslim kama zawadi. Vile vile tumetoa simu 30 na gari moja aina ya Renault Kwid yenye thamani ya 23m/-.
Kwa kumalizia Ikunda aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na akatamka kwamba baada ya promosheni hiyo kuisha, Tigo wamezindua nyengine,ambayo itachukua vile vile mda wa miezi mitatu na mshindi atatangazwa kupitia vyombo vya habari,kama waliopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...