Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Kondoa imejipankuendelea kutoa chanjo ya magonjwa ya Mifugo kulingana na kalenda ya chanjo inavyoonyesha kwa mwaka mzima.
Hayo
yalibainishwa na Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Mji Bi. Monica
Kimario wakati wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa Kimeta na Chambavu kwa
mifugo ya kata ya Kingale.
“Nawasihi
sana wafugaji wa Kata ya Kingale washiriki katika zoezi hili kwa kuleta
mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya utoaji wa chanjo ili
kudhibiti magonjwa yatakayotokea bila kufanya hivyo mifugo
itashambuliwa na magonjwa hayo,”alisema Bi. Monica
Aidha
aliwashauri wafugaji kuleta mifugo yao yote waliyonayo ili kupata
chanjo kwani baadhi ya wafugaji huleta mifugo michache kupata chanjo na
kuficha mingine hali inayohatarisha kutokea kwa magonjwa kwa mifugo
ambayo haitapata chanjo.
“Chanjo
hii ni salama kabisa na inatolewa na wataalam wa mifugo na hakuna
matatizo yoyote yaliyotolewa kwa maeneo ambayo chanjo imetolewa na
nawahisi wafugaji kutumia wataalam wa mifugo katika matibabu ya mifugo
yao ili kuepukana na kupewa chanjo isiyo sahihi na hatari kwa mifugo
yao,”alisisitiza Bi. Monica.
Hata
hivyo alitaja faida za mifugo kupatiwa chanjo kuwa ni pamoja na
kudhibiti magonjwa, kuongeza uwezo wa wanyama kujikinga na maradhi,
kupunguza gharama za matibabu na kuzuia magonjwa ya kuambukiza kutoka
kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
“Hasara
za kutopata chanjo nazo zipo ambazo ni kupoteza mifugo kwa vifo,
kupunguza uzalishaji wa mifugo na uambukizaji wa magonjwa ya mifugo
kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu,”alibainisha Bi. Monica.
Halmashauri
ya Mji Kondoa imejipanga kuhakikisha wanapunguza vifo vya mifugo na
kuongeza uzalishaji kwa kutoa chanjo ambapo kwasasa imeanza kutolewa
katika kata ya Kingale kwa magonjwa ya Kimeta na Chambavu ambapo kwa
Halmashauri yote jumla ya ng’ombe 26,696, mbuzi 18,417 na kondoo 2782
wanatarajia kuchomwa chanjo hiyo.
Afisa
Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Kondoa Bi. Monica Kimario akivuta
dawa tayari kwa kuanza zoezi la utoaji wa chanjo kata ya Kingale
Mwananchi
akiwa akivusha sanduku la kuhifadhia dawa za chanjo tayari kwenda kutoa
huduma kwa wafugaji wanaoishi upande wa pili wa mto
Wataalam wakivuka maji ya mto Bubu kwa ajili ya kwenda kutoa chanjo kwa wafugaji wanaoishi upande wa pili wa mto huo
Daktari wa Mifugo kutoka
Idara ya Mifugo Halmashauri ya Mji Keneth Makunga akimchoma sindano
ng’ombe aliyeletwa kwa ajili ya chanjo.
Afisa Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji akitoa risiti ya mfumo kwa wafugaji waliofika kwa ajili ya mifugo yao kupata chanjo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...