Editha Karlo,Kigoma.
ASASI ya kijamii ya Inspirational women Group wametoa msaada wa taulo za kike kwa kushirikiana na shirika la msalaba mwekundu Tanzania (red Cross)na wadau mbalimbali kwa wanafunzi wa kike 150 wa sekondari ya Wakulima iliyopo Mkoani Kigoma katika Manispaa ya Kigoma ujiji.
Akitoa mada juu ya hedhi salama kwa mtoto wa kike Mwenyekiti wa women inspirational Aisha John kabla ya kugawa taulo hizo alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani muda wote na waweze pia kusoma kwa utulivu na kujiamini.
Alisema suala la hedhi kwa mtoto wa kike ni suala la kawaida na si jambo la aibu au laana bali ni hatua za ukuaji za kimwili.
"Sisi wanawake tunajivunia sana tunapoingia hedhi kwani tunakuwa na uhakika tunaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto hivyo suala la hedhi siyo la aibu au laana"alisema
Pia aliwataka wanafunzi hao wanapoingia kwenye hedhi kuzingatia usafi kwa kuzifua taulo hizo kabla ya kuzitumia kwa mara nyingine.
Aliongeza kwa kusema kuwa ikiwa sasa hivi dunia inaelekea katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika tarehe 8 mwezi wa tatu na mwaka huu Kitaifa inafanyika Simiyu na ujumbe wake ni "kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadae"wameamua kusherekea siku hiyo na wanafunzi wa kike kwa kuwapatia taulo hizo ili wanapokuwa kwenye hedhi wasijisikie wanyonge.
Alisema katika kampeni hii ya kuhamasisha hedhi salama kwa mtoto wa kike ni endelevu na itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja wamechagua shule tatu za sekondari kuanza nazo kwenye mpango huo ambazo ni Buteko Sekondari,Buhanda sekondari na Wakulima sekondari.
Mratibu wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania kwa Mkoa wa Kigoma(red cross)Khalid Selemani Ausii akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi hao alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani na uhuru muda muda wote na wao kama chama wapo tayari kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali.
Alisema watoto wakike wanapokuwa kwenye hedhi zao wanatakiwa wasijisikie wanyonge kwa kukosa taulo za kike na kushindwa kuhudhuria masomo yao kwa ukamilifu.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari ya Wakulima William Siumbe Diara aliwashukuru insparation women Group pamoja na wadau walioshiriki kuwasadia watoto wa kike shuleni hapo kwa kuwapatia taulo za kike kutawafanya kusoma kwa kujiamini.
"Mmefanya jambo zuri salama tunawashukuru tunaomba hiki kitu kiwe endelevu kwani itawasaidia wanafunzi wa kike kuwa na uhakika wa masomo hata wanapokuwa kwenye hedhi na kuacha tabia ya kushindwa kuja shule sababu ya hedhi"alisema
Alisema msaada huo wa taulo za kike umekuja wakati muafaka na niwamaana kubwa na taulo hizo ndo zinafaa kulingana na mazingira kwakuwa mahudhurio ya shule kwa kila mwezi kwa watoto wa kike yanakuwa siyo mazuri kwasababu ya kushindwa kumudu gharama za taulo wanapokuwa kwenye hedhi.
Mwalimu mkuu huyo alisema shule yake inachangamoto ya upungufu mkubwa wa waalimu wa kike hali inayofanya waalimu wa kiume kusaidia kutoa huduma kwa watoto wa kike.
"Shuleni hapa tuna jumla ya waalimu 18 ambapo kati ya hao mwalimu wa kike ni mmoja tu lakini taarifa hii nimeshaiwakilisha kwa mwajiri wangu ambaye amehaidi kulifanyia kazi jambo hili"alisema.Aliitaja sababu kubwa inayochangia shule hiyo kukosa waalimu wa kike ni umbali wa kutoka stand ya magari na kufika shuleni.
"Hapa hatuna nyumbani za waalimu,kumpata mwalimu wa kike kila siku atembee umbali unaotumia dakika 30 hadi kufika hapa ni kazi ila mwajiri wangu analifanyia kazi suala hili"alisema
Naye Mwanafunzi Imaculate Maico wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya wakulima anasema wamekuwa wanakutana na changamoto wanapo kuwa kwenye hedhi huwalazimu kurudi nyumbani huku masomo yanakuwa yanawapita.
"Tunajisikia wanyonge tunapoingia kwenye hedhi na kukosa taulo za kike,ila sasa hivi hali itakuwa tofauti baada ya kupewa zile mada juu ya hedhi salama pamoja na kupewa taulo hizi tutajiamini na kuuhudhuria masomo kikamilifu"alisema
Uongozi wa inspirational women Group na wanachama wake wakiwa wameshika taulo za kike kabla ya kuwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mkulima
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya mkulima wakifuatilia mada mbalimbali juu ya hedhi salama
Mratibu wa shirika la msalaba mwekundu Tanzania(red cross)wa Kigoma Khalid Selemani Ausii akitoa neno kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya wakulima juu hedhi salama
Mwenyekiti wa Inspirational women Group akitoa mada ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Wakulima iliyopo katika Manispaa ya Kigoma ujiji.
Wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Wakulima wakifurahia taulo za kike walizopewa na insperational women group kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwaajili ya hedhi salama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...