Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitolea ufafanuzi hoja
zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii kuhusiana na mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha
Ardhi Tabora wakati kamati hiyo ilipokwenda kukagua maendeleo ya mradi
huo mwishoni mwa wiki . Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati Kemilembe Lwota na
kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Magdalena Sakaya akiwasilisha hoja
kuhusiana na Mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora
mwishoni mwa wiki wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua maendeleo ya
ujenzi wa mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nicolaus Mkapa akijibu moja ya hoja
zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora. Wa pili kulia ni Kamishna wa Ardhi
Nathaniel Methew Nhonge na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya
Ardhi Hamdoun Mansoor
Jengo la Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora ambalo ujenzi wake umesimama kutokana na changamoto mbalimbali.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Nape Nnauye akisalimiana na Kamishna
wa Ardhi Nathaniel Methew Nhonge wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi
Tabora. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
***************************
Na Munir Shemweta, WANMM TABORA
Kamati ya Bunge
ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeamua kuubeba mradi
wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora kilichopo mkoani Tabora
kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unapatiwa fedha za kutosha na
kukamilika ili kukiwezesha chuo kuwa na Maktaba kubwa na ya kisasa.
Uamuzi huo wa
Kamati unafuatia kuelezwa kuwa, ujenzi wa mradi wa Maktaba ya Chuo cha
Ardhi Tabora umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya
fedha pamoja na na majadiliano ya muda mrefu kati chuo na Mshauri
Msimamizi wa ujenzi ambaye ni Wakala Ujenzi Tanzania (TBA).
Akizungumza
mwishoni mwa wiki mkoani Tabora wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Ardhi, Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo,
Mwenyekiti wa Kamati Kemilembe Lwota alisema, kamati yake imeamua
kuubeba mradi huo kama suala maalum na kulipeleka mbele zaidi na
kuhakikisha kama kamati wanaifanya kazi hiyo kwa uhakika ili kusaidia
kukamilika kwake.
‘’Hata hiki
kizuri kilichokuja cha kujenga maktaba mlichoanza kukitengeneza lakini
ndani ya miaka mitano ujenzi umesimama kweli kuna shida, naungana na
wajumbe wenzangu hili suala tutalichukua kama issue mahsusi ya kamati na
tutalipeleka mbele zaidi na kufanya kazi hiyo kwa uhakika na umakini
zaidi’’ alisema Kemilembe.
Mbunge wa jimbo
la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye ameshangazwa na mradi wa ujenzi wa
maktaba hiyo kutokamilika kwa wakati pamoja na kamati hiyo kusaidia mara
kadhaa kujenga hoja za kusaidia upatikanaji fedha. Ameitaka Serikali
kuhakikisha fedha za ukamilishaji ujenzi huo zinapatikana.
Naye Mbunge wa
jimbo la Kaliau mkoani Tabora Magdalena Sakaya alisema, pamoja na
Tanzania kuwa na vyuo vya ardhi viwili (Morogoro na Tabora) vinavyotoa
wahitimu wa ngazi ya Cheti na Diploma lakini kutokamilika kwa mradi wa
Makataba ya Chuo hicho unachangia migogoro ya ardhi inayosababishwa na
ukosefu wataalamu wa kutosha katika fani mbalimbali za ardhi.
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaeleza
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii
kuwa, changamoto iliyosababisha kutokamilika mradi wa ujenzi wa Maktaba
ya chuo cha ardhi Tabora kwa wakati ni upatikanaji mafungu ya fedha
kutokuja kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo, Dkt
Mabula alisema pamoja na changamoto hiyo chuo kimeendelea kufanya vizuri
katika utendaji kazi ikiwemo kuongeza udahili kila mwaka na kubainisha
kuwa katika jitihada za kukijengea uwezo wa chuo Wizara imekipa mradi wa
kuzalisha baadhi ya nyaraka zinazohusiana na masuala ya ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...