Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blogu ya Jamii
KAMISHNA wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, amewasili mkoani Singida na kisha kutumia nafasi hiyo ufafanuzi kuhusu matukio ya mauaji ya watu 14 yaliyotokea wilayani Manyoni mkoani humo kuanzia mwaka jana mpaka Februari mwaka huu huku akitoa maagizo ya kutafutwa na kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
KAMISHNA wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, amewasili mkoani Singida na kisha kutumia nafasi hiyo ufafanuzi kuhusu matukio ya mauaji ya watu 14 yaliyotokea wilayani Manyoni mkoani humo kuanzia mwaka jana mpaka Februari mwaka huu huku akitoa maagizo ya kutafutwa na kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
Akizungumza leo mkoani Singida Kamishna Sabas amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hizo za uongo ambazo zilisambazwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na hivyo amemtaka kujisalimisha katika kituo chochote cha Polisi, huku akitoa maagizo kwa Kamanda Polisi Mkoa wa Singida kumtafuta Lema popote alipo na akamatwe.
Kamishna Sabas amesema Februari 29 mwaka huu huko katika Wilaya ya Manyoni wakati wa kutoa salamu kabla ya mazishi ya marehemu Alex Jonas aliyekutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake katika eneo la Mbugani, Godbless Leama alionyesha orodha ya watu 14 ambayo pia aliiweka katika mitandao ya kijamii akidai waliuawa kwa kuchinjwa wilayani Manyoni bila ya kuwa na uhakika kama taarifa hizo ni sahihi huku akilituhumu Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Akifafanua kuhusu matukio hayo Cp Sabas ameeleza ukweli wa matukio hayo ni kwamba Sichelela Mosses, (22), ambaye ni Mkazi wa Sayuni alikutwa ameuawa Agosti 13 mwaka 2019 majira ya usiku huko maeneo ya Mnarani barabara ya kuelekea Itigi.
“Binti huyo alikutwa ameuawa na baada ya uchunguzi ilibainika kuwa mauaji hayo yametekelezwa na mume wake aitwaye Rashidi Hamisi akishirikiana na Timoth Leonard, sababu ikiwa ni wivu wa mapenzi kwa kumtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi watu wengine. Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa pamoja na vielelezo vyote vilitumika kwenye mauja hayo,”amesema.
Pia amesema Abdallah Lyama, (38), mkazi wa Kihanju, Itigi, alifariki dunia Agosti 26 mwaka 2019, saa 2 usiku wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya St. Gaspar Itigi, wilayani Manyoni kutokana na shambulio la kupigwa kwa fimbo pamoja na mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na Rajabu Juma(42) akishirikiana na Haruna Hamisi, kwa pamoja walikuwa wanamtuhumu marehemu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa dada yake Rajabu Juma, aitwaye Asha Miraji(19).
Amesema tukio hilo lilitokea Agosti 25 mwaka 2019 huko maeneo ya Mji Mpya, Itigi walipomvizia marehemu akiongea na Binti huyo kichochoroni. Mtuhumiwa Rajabu s/o Juma amekamatwa na juhudi za kumtafuta mwenzake zinaendelea.
Kamishna Sabas amesema tukio lingine ni la Rajabu Abasi(36)aliyefariki dunia Septemba 14 mwaka 2019 usiku akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Gaspar, Itigi kutokana na tukio la kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtuhumiwa aitwaye Mohammed Abdi.Tukio hilo lililotokea Septemba 13 mwaka 2019 saa 3 usiku huko katika Kijiji cha Mwamagembe.
“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa alimfumania marehemu akiwa na mke wake nyumbani kwa mtuhumiwa. Mtuhumiwa amekamtwa na upelelezi umekamilika,”amesema Kamishna Sabas.
Pia Martini Motekwa anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, ambaye inasadikiwa kuwa ana upungufu wa akili na akiwa hana makazi maalum, mwili wake ulikutwa kwenye kibanda alichokuwa akijihifadhi nyakati za usiku ukiwa umechomwa moto. Katika uchunguzi mwili huo pia ulibainika kuwa na jeraha kichwani ambalo linasadikiwa kusababishwa na kitu chenye ncha kali. Bado uchunguzi wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea
Kamishna Sabas amesema kuwa Hamad Hussein, (37), mkazi wa Manyoni alifariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi wanaosadikiwa kujichukulia sheria mikononi kwa kutumia fimbo na mawe kutokana na tuhuma za wizi wa mifugo. Mtuhumiwa mmoja aitwaye Hussein Mrisho amefikishwa mahakamani kuhusiana na tukio hilo.
Akiendelea kufafanua kuhusu matukio hayo ya maujiaji Kamishna Sabas amesema kuwa Emmanuel Meso, (50), Mkazi wa Kijiji cha Maweni, Tarafa ya Kintinku, alifariki dunia kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za siri. Mwili wake uligundulika Novemba 8 mwaka 2019 alifajiri ukiwa umetupwa porini. Katika uchunguzi wa Polisi imebainika kuwa watu nane wanasadikiwa kuhusika katika kutenda kosa hilo linalohusishwa na imani za kishirikiana.
Aidha katika tukio hilo yupo Mganga wa Jadi anayesadikiwa kuwatuma watuhumiwa kuchukua shemu hizo za siri. Watuhumiwa wote wamekamatwa na upelelezi umekamilika, waliokamatwa ni Abdul Muhengwa, Henry Madinda, Stephano Ligoha, Juma Kassim, Makayola Gaudence, Regina Jacob, Wami Ngalya, na Anderson Sabini.
Pia Mika Saimon, (38), alifariki dunia kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili katika tukio lililotokea Novemba 15 mwaka 2019 saa 10 jioni huko Kitongoji cha Idodoma katika tarafa ya Nkonko, ambapo marehemu aliuawa na mtoto wake aitwaye Saimon Mika kwa akishirikiana na mama yake mzazi aitwaye Mea Mwarabu pamoja na rafiki wa mtoto wake aitwaye Robert Elia ambapo walikuwa wanataka kurithi shamba la baba yao. Watuhumiwa wote watatu wamekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.
Tukio lingine la mauaji linamhusu Mshoma Ngassa, (30), Mkazi wa Itigi alifariki dunia kwa kupigwa kwa fimbo kichwani na mume wake aitwaye Mariyambelele Senzo katika tukio lililotokea tarehe 21/11/2019 saa 2:30 asubuhi huko Majiweni, Kata ya Mitundu ambapo chanzo cha kifo ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa akimtuhumu mke wake kutembea na mwanaume ambaye bado hajafahamika. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.
Pia John Logion, (60), Mkazi wa Mitundu alifariki dunia katika tukio lililotokea tarehe 22/11/2019 saa 11 jioni kwenye shamba la mihogo, lilnalomilikiwa na Anthony Lipiti huko Itigi. Uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wizi ambapo marehemu alikwenda kwenye shamba la mtuhumiwa kwa nia ya kuiba mihogo na mtuhumiwa kutumia mwanya huo kumshambulia kwa kumpiga na kitu kizito kichwani. Mara baada ya tukio mtuhumiwa alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea kwa kushirikiana na Viongozi wa Eeneo husika.
Katika matukio hayo ya mauaji Kamishna Sabas amesema Michael Charles, (35), Mkazi wa Mwamagembe alifariki Januari 1 mwaka 2020 wakati anapatiwa matibabu katika Zahanati ya Mwamagembe, Itigi kutokana na taarifa za kujeruhiwa na Fatuma Ramadhani na tukio lililotokea tarehe Desemba 21, 2019.
Katika tukio hilo inasadikiwa kuwa Fatumaa d/o Ramadhani ambaye ni Mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi marehemu alimpiga kwa jiwe kichwani na kisha kumvuta sehemu za siri kutokana na ugomvi wa uchafuzi wa mazingira katika eneo la nyumba wanayoishi. Hata hivyo tukio la kujeruhiwa halikuripotiwa Polisi hadi muathirika alipofariki. Baada ya tukio la kujeruhi mtuhumiwa alotoroka juhudi za kumtafuta zinaendelea.
“Issa Abdallah (2), ambaye alikuwa mlemavu wa miguu alifariki dunia tarehe 24/1/2020 saa 12 jioni huko katika Kitongoji cha Ibonoa, Kata ya Sanjaranda – Itigi kutokana na kunyongwa na mama yake mzazi kwa kile kinachodaiwa kukosa mahitaji kutoka kwa baba wa mtoto aitwaye Abdallah Muna, (56), Mnyaturu aliyemtelekeza bila matunzo. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.
“Jumanne Ndelemo, (22), alifariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na kaka yake wake aitwaye Hamisi s/o Ndelemo, kutokana na kumfumania akiwa na mke wake. Tukio lilitokea Februari 5 mwaka 2020 saa 3:30 usiku huko katika Kijiji cha Makasuku, huko Sasajila na mtuhumiwa amwekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika,”amesema.
Pia Kamishna Sabas ameeleza kuwa Heri Mamba alifariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki yenye namba za usasjili MC 273 CDK aina ya FEKON. Kutokana na uchunguzi wa awali wa Polisi imebainika kuwa marehemu alikuwa amelewa huku akikatiza barabarani bila kuchukua tahadhari. Mtuhumiwa Ombeni s/o Chanzi, Mgogo, (35), mkazi wa Chinyika amekasmatwa na amekiri kutenda kosa hilo na si kuchinjwa kama ilivyodaiwa kwenye malalamiko.
“ Alex Jonas, (40), dereva bodaboda, aligundulika kufariki dunia Februari 26 mwaka 2020 saa moja asubuhi na chunguzi unaendelea ili kuweza kubaini chanzo cha kifo cha marehemu pamoja na wahusika wa tukio hilo.Katika taarifa ni za upotoshaji zenye lengo la kuleta taharuki kwa Jamii pamoja na kuwachonganisha Wananchi na Jeshi lao la Polisi,”amesema.
Kamishna Sabas amesema kuwa hakuna mwanasiasa au mtu yoyote atakaetumia Jeshi la Polisi kama kimvuli cha kujipatia umarufu, huku akiwaonya anasiasa wanaojifanya kuwa ni wasemaji wa Jeshi la Polisi amewaonya na kusema kuwa jeshi halitamvumilia mtu au kiongozi yoyote atakaeichafua serikali kwa namna moja au nyingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...