* Kauli ya Rais Magufuli ya Uchaguzi mkuu  kuwa huru na haki yawafurahisha vyama vya siasa

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amesema kuwa Rais Dk.John Magufuli amewathibitishia vyama vya upinzani nchini Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba utakuwa wa huru na haki.

Mbatia ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk.John Magufuli ambapo katika mazungumzo yao moja ya jambo ambalo wameligusia ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

"Leo tumekutana na Rais, tulimuomba kukutana naye, na sababu kubwa tulitaka kuthibutisha kutoka kwake kuhusu kauli yake ambayo aliitoa kwa mabalozi kuwa uchaguzi wa mwaka huu .Rais ametuthibitishia kweli ile ni ya kweli na ataisimamia kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na haki,"amesema Mbatia.

Amesisitiza kwamba Rais Magufuli kauli yake haina hiyana  na ni ya kweli ,hivyo ni jukumu la Watanzania wakiwemo wanasiasa kuhakikisha wanafuata misingi iliyopo kwa mujibu wa Katiba katika kutekeleza shughuli za kisiasa na kubwa zaidi kwa umoja wetu ni kuendelea kuifanya nchi ya Tanzania kuwa salama.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Watanzania,wanasiasa kuwataka wawe wanazungumza zaidi mambo yanayohusu nchi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na kwamba hakuna sababu ya kuendeleza malumbano na mabishano yasiyokuwa na tija.

'Viongozi tulioko kwenye vyama vya siasa  nchini tuwe tunashindana kwa hoja,kwa mfano hivi sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu  na kila Chama cha siasa kitakuwa na Ilani yake ya uchaguzi, hivyo ni vema Ilani hizo zikazingatia misingi ya nchi yetu  na mahitaji ya muhimu kwa maendeleo ya Watanzania,"amesisitiza Mbatia.

Ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa vyama vingi nchini lakini kuna kila sababu ya kutanguliza Taifa mbele badala ya vyama vya siasa huku alisisitiza kuna mambo mengi ya msingi ambayo Watanzania wanahitaji kuona yakifanywa na vyama vya siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...