Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo nchini Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema wanatarajia kuanzisha kliniki za kutoa ushauri wa ufugaji katika kila Halmashauri ili kuongeza thamani ya ngozi inayozalishwa.

Profesa Gabriel ameyasema hayo  leo Jumamosi Machi 7, 2020  wakati wa kufungua mkutano wa wadau mbalimbali wa sekta Mifugo  jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Mkutano huo ni  vyama vya Wafugaji Kuku  Nguruwe  pamoja na wadau wa ngozi uliolenga kupokea changamoto za  katika Biashara  Biashara ili  zitafutiwe ufumbuzi.

Profesa Ole  Gabriel amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanunuzi kuwa kuna baadhi ya ngozi haikidhi viwango vya ubora unaotakiwa katika uzalishaji bidhaa jambo ambalo limekuwa likiikosesha serikali mapato.

“Sasa ili kukabiliana na suala hili, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) tutashirikiana  katika hatua mbalimbali ili kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na kliniki ya mifugo,” amesema Profesa Ole Gabriel.

Profesa Ole Gabriel amesema katika sehemu ya  mfugaji ataweza kupata elimu ya namna ya kutunza mifugo yake huku akitolea mfano wa ng’ombe kuanzia akiwa na mimba, baada ya kuzaa na namna ya kumtunza hadi anakuwa mkubwa ili aweze kuleta faida inayokusudiwa na wafugaji pamoja na serikali kupata mapato sitahiki.

“Suala la utunzaji wa mifugo inayozalisha ngozi litaenda hadi katua za  uchinjaji ambapo visu maalumu vitasambazwa katika maeneo na elimu maalumu ya uchunaji na elimu italolewa  inayozingatia viwango vya upatikanaji ngozi bora,” amesema

Mwenyekiti wa Wadau wa ngozi Tanzania, Adam Ngamilo ameonyesha kufurahishwa na uamuzi wa serikali huku akibainisha kuwa utawasaidia katika kuboresha mnyororo wa thamani za bidhaa.

“Suala hili lilikuwa ni changamoto sana kwetu hasa sisi viongozi tunaomaliza muda tunaamini watakaoingia wataitumia ipasavyo,” amesema Ngamilo

Kwa upande wa wafugaji wa kuku wameiomba Serikali kuwasaidia kupata mitaji ili waweze kufanikisha malengo yao.

“Tunaiomba Serikali itusaidie kupata mitaji ambayo kupitia mikopo ya riba nafuu ili tuweze kufika mbali na kutoa fursa za ajira kaa watu wengi zaidi,” amesema Denis Joseph ambaye ni mfugaji wa kuku

Akijibu hoja hiyo, Katibu mkuu huyo amesema atahakikisha pia anazungumza na katibu mkuu wa Tamisemi ili asilimia kumi inayotengwa katika kila halmashauri iweze kunufaisha wafugaji wadogo ikiwamo wakina mama na vijana.

Kwa sasa sheria inazitaka halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu. 



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel  akizungumza wakati wa  mkutano vyama vya wafugaji kuku na nguruwe uliolenga kupokea changamoto ili zitafutiwe ufumbuzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wadau wa Kuku Tanzania, Harko Bhagat akitoa changamoto tatu wanaziozipata kwenye ufugaji wa kuku kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel(hayupo pichani) wakati wa  mkutano vyama vya wafugaji kuku na nguruwe pamoja uliolenga kupokea changamoto ili zitafutiwe ufumbuzi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa TAPIFADorin Maro akitoa changamoto wanazokutana nazo kwenye ufugaji wa Nguruwe kwa wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel(hayupo pichani) wakati wa  mkutano vyama vya wafugaji kuku na nguruwe uliolenga kupokea changamoto ili zitafutiwe ufumbuzi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafugaji wa kuku na nguruwe pamoja na wauzaji wa vyakula vya mifugo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel  alipokuwa anafungua mkutano vyama vya wafugaji kuku na nguruwe uliolenga kupokea changamoto ili zitafutiwe ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel(katikati) akizungumza wakati wa kufungua mkutano wadau wa ngozi uliolenga kuchagua viongozi wapya wa Chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wadau wa ngozi Tanzania, Adam Ngamilo.
Baadhi ya wadau wa ngozi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel  alipokuwa anafungua mkutano kwa ajili ya kuchagua uongozi mpya
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wadau wa ngozi Tanzania, Adam Ngamilo akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa ngozi waliokutana kwa ajili ya kuchagua uongozi mpya. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Ngozi mara baada ya kufungua mkutano wao uliokuwa unahusu kuchagua uongozi mpya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...