*THTU yataka wanawake kufanya kazi kwa umahiri pindi wanapopata nafasi

*Maafisa Rasilamali watakiwa kufuata sheria za upandishaji Vyeo

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Wanawake  wengi waliopata nafasi wameonyesha uwezo wa kufanya vizuri hali ambayo imefanya kubaki katika nafasi zao ikilinganishwa na wanaume kwa kipindi cha miaka mitano.

Hayo aliysema Katibu wa Tawala Wilaya Ilala Jabir Makame katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa Chuo cha Biashara (CBE). Makame ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema amesema Wanawake ni wana uthubutu katika kufanya Kazi.

Amesema kwa mwaka huu wa uchaguzi Wanawake watumie nafasi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweza kuingia kwenye kufanya maamuzi.

Maadhinisho hayo yaliratibiwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa Kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU).

Amesema Serikali imeweka mazingira mazuri kwa Wanawake kwa kuwepo kwa Makamu wa Rais pamoja ngazi mbalimbali za uongozi wanawake wapo.

Aidha amesema serikali imeweka mazingira ya kuwepo kwa mikopo ya Wanawake na fedha zipo na kutaka  wanawake kwa kuendeleo imara kwa kuwa wazalishaji mali pamoja.

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa  Kamati ya Wanawake  Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  Salma Fundi amesema kuwa THTU inatambua serikali imetunga sheria, miongozo na kanuni  ambazo kama zingetekelezwa vizuri basi tunauhakika asilimia 70  ya matatizo au kero za Wafanyakazi zingeweza kupungua na baadhi ya kero  kuisha kabisa.

Amesema kuwa kuna   ucheleweshaji wa Kupandishwa Madaraja kutokana na uzembe na ushauri mbaya kwa waajiri kutoka kwa  bàadhi Maafisa Rasilimali Watu kutowapandisha watu kwa wakati kwenye mfumo wa LOWSON pindi mtu anapofikisha sifa za kupandishwa, yaani miaka minne lakini mafanyakazi huyo anaweza kubaki kwenye cheo kimoja kwa miaka mingi bila kupandishwa  wakati miongozo ipo .

 Fundi amesema kuna upendeleo au ubaguzi,  kupandisha watu vyeo, na wakati mwingine kuwapandisha watu  bila kuwaingiza kwenye bajeti za vyuo, kutokupandisha malimbikizo ya watu kwenye mfumo wa LOWSON kwa wakati na kufanya watu wakose malipo hayo, kutoa vyeo vya kukaimisha bila kufuata utaratibu na kuwafanya watu wakose haki zao, kushindwa kutekeleza Waraka wa Msajili wa Mwaka 2015 ambao unaelekeza haki ya mtu kuombewa tofauti ya mshahara wake wa awali kama mshahara binafsi na kusababisha manunguniko mengi.

“ Alitoa wito Wanawake kuacha kurudi nyuma na kusema Uongozi ni Kazi za Wanaume wakati uwezo wa kufanya wanao. chukueni  fursa zilizopo, ni Haki yetu ikiwemo kugombea nafasi za Uongozi wa Siasa katika Mwaka huu wa Uchaguzi. Mwisho nawakumbusha wanawake kama tunataka kufikia hamsini kwa hamsini tusisahau kuwawezesha wanawake wenzetu Kama tukiweza kufanya kila mwanamke kiongozi asaidie kunyanyua mwanamke mmoja au wawili kushika madaraka basi tutaweza. Walimaliza kwa kusema wanawatakia  maadhimisho mema wanawake wote na kuwaombea kwa kusema anawapenda sana wanawake wote na Mungu Aibariki Tanzania, Mungu Awabariki Wanawake Wote”.Amesema Fundi

Kamati ya wanawake kuelekea  maadhimisho ya  siku ya wanawake Duniani  ya mwaka 2020 tumeandaa kongamano la kuwajengea Wanawake uwezo wa  kielimu katika masuala ya uongozi lakini pia tumeweza  kujadili kwa pamoja, Changamoto zetu na kufikiria  suluhisho la kuwa tunaiomba serikali itusaidie changamoto za Maafisa Rasilimali Watu na Waajiri na kutaka kuwa a utaratibu wa ukaguzi (Auditing) kwenye majukumu yao kwa mwaka ili kubaini ukiukwaji wa utaratibu uliowekwa.

Kamati hiyo  ilikipongeza Chuo cha Biashara (CBE) kuwa na mwanamke kama Naibu Mkuu wa Chuo ambapo walitaka na vyuo vingine vifanye hivyo pale ambapo  wanawake wenye sifa na uwezo wapo kwenye taasisi basi wapewe nafasi. Hii itasaidia utekelezaji wa nia njema ya serikali ya awamu ya tano ya kuleta usawa katika nafasi mbali mbali za uongozi na wasimuachie Mheshimiwa Rais atekeleze peke yake.

Fundi amesema wanawake wafanye kazi  kwa kuzingatia Uadilifu na Umahiri wa kufanya kazi kwa bidii pale  tunapopata nafasi za uongozi ili kujitofautisha na wa akina Baba katika utoaji huduma kwani ni asili yetu kuhudumia na kuongeza kuwa wanawake wenyewe ifikie hatua Sasa tuseme kuwezeshwa   imetosha na tujipange kwa kuongeza weledi na uthubutu wa kutafuta fursa kwani mazingira rafiki yapo ya kutufanya kupata nafasi za uongozi ili mradi tutafute sifa za kutuwezesha.

 “Tunamaanisha tuhudumie watu bila ubaguzi ikiwemo watu wasiojiweza kama vile  Walemavu, Watoto, Wazee, Wagonjwa na Maskini, kea kufanya hayo itatufanya tukubalike kwenye jamii katika uongozi lakini pamoja na kufikia  malengo ya Siku ya Mwanamke Duniani kwa kuonyesha mchango wetu katika jamii. Kwa upande  wazalishaji mali kamati inasiaitiza wanawake tushirikiane sana katika ujasiriamali pia, kwani ndiyo njia pekee itakayotuongezea kipato, cha msingi ni  kuwa na malengo na nidhamu ya pesa”.amesema Fundi
 Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilala Jabiri Makame akizungumza  katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kwa Wafanyakazi wanawake wa Chuo cha Biashara  (CBE) kwa  na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  maadhmisho yalifanyika katika wa Chuo cha Biashara  (CBE) jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Wanawake  Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  Salma Fundi  akizungumza na wafanyakazi wanawake wa Chuo cha Biashara  (CBE) kuhusiana masuala ya wanawake na changamoto katika ajira.
 Makamu Mkuu wa Chuo  Taaluma wa Chuo cha Biashara (CBE)  Profesa Edda Luoga akizungumza kuhusiana na wanawake wanavyotoa mchango katika maendeleo katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yalifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 .Katibu wa Kamati ya wanawake Taifa wa wanachama wa Chama ambao ni wanawake wa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU) Roselyne Masam akisoma lisala kwa mgeni rasimu kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wanawake duninia kwa chuo cha Biashara (CBE).
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Wanawake  Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  Salma Fundi (Mwenye tisheti) akiteta na wanachama wa THTU katika maadhimisho  ya siku ya wanawake katika yaliyofanyika katika chuo cha Biashara (CBE)
Baadhi ya wanawake wakiwa katika maadhimisho Chuo cha Biashara (CBE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...