

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
Mbunge wa Jimbo la
Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa amekabidhi viti mwendo kwa
watoto wenye ulemavu wa miguu katika jimbo lake.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi viti mwendo hivyo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa, viti mwendo
hivyo ni msaada kutoka kwa mama Janeth Magufuli hivyo anakabidhi kwa
walengwa ili kutimiza wajibu wake kama alivyooagizwa na mama Janeth
Magufuli.
Alisema Viti mwendo
hivyo vitawasaidia watoto hao kutembea sehemu mbali mbali kwa kuendesha
wenyewe au kuendeshwa na kuondoa usumbufu wa kuwabeba hata pale
wanapokuwa na safari za lazima kama vile Hospitali Nk.
Aidha, aliwataka
wazazi na walezi kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuwahudumia watoto
hao kwa muda mrefu zaidi jambo ambalo litampa moyo yule aliyetoa na
kufikiria kutoa msaada mwingine.
Katika hatua nyingine
Mbunge huyo wa Jimbo la Bagamoyo aliwashauri kina mama wenye watoto
walemavu kuunda kikundi na kukisajili ili waweze kupatiwa mikopo ya
serikali inayotolewa kwa vikundi.
Alisema serikali
haiwezi kusaidia wananchi mmoja mmoja hivyo ni vyema wakiwa kwenye
kikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ambayo haina
riba na kwamba itawasaidia kujiendeleza kulingana malengo
watakayojiwekea.
Dkt. Kawambwa alitoa
rai hiyo baada ya kina mama wenye watoto walemavu kumuomba awasaidie
wapate mitaji kwa ajili ya biashara ili kukabiliana na malezi ya watoto
hapo.
Kwa upande wao wazazi
na walezi wa watoto hao walimshukuru Mbunge huyo kwa kufikisha viti
hivyo kama alivyokabidhiwa na mama Janeth Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...