NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
Jeshi la Polisi jijini
Mwanza, limefanikiwa kumtia mbaroni kinara wa usafirishaji na muuzaji
wa dawa za kulevya aina ya mirungi, Peter Charles Mwita alimaaarufu Peter Mirungi (46) mkazi
wa Mtaa wa Rufiji, kwa makosa ya kusafirisha, kusambaza na kuuza mirungi jijini
Mwanza.
Mbali na Peter jeshi
hilo linawashilia watu wengine wawili kwa tuhuma za namna hiyo huku mmoja
akiwakimbia polisi baada ya kuruka kutoka ndani ya gari alilokuwa akiliendesha
kwenye kizuizi cha Ngashe Kata ya Lugeye, wilayani Magu.
Mtuhumiwa huyo ambaye
amelisumbua jeshi hilo ka miaka mingi baada ya kubaini anafuatiliwa na polisi, Februari 1, mwaka huu alitelekeza
gari lake namba T.787 DQX aina ya Probox eneo la Igoma Mashariki, likiwa na
mirungi kg 9.02.
Pia Februari 15, Peter ambaye amekuwa akifanya biashara
hiyo haramu kwa muda mrefu baada ya kuwakimbia polisi aliangukia na mkono wa
dola.
Aidha Machi 2, mwaka
huu majira ya 12:00 asubuhi huko kwenye
kizuizi cha magari kilichopo Katika Kijiji cha Ngashe, Kata ya Lugeye, wilayani
Magu, askari wa doria walikamata bhangi kg 50, zikiwa kwenye magunia matatu, ndani ya gari lenye namba za usajili T.881 AFX
na tela namba T.822 CZZ Lori aina ya scania.
Gari hilo
lilikuwa likitokea Tarime kuja jijini Mwanza, likiendeshwa na dereva
aliyetambulika kwa jina la Joseph Achiyo ambaye aliruka kwenye gari na kukimbia
baada ya kusimamishwa na askari. 28
Pia Faustine Koroso (46)
mkazi wa Nyakato Mashariki na Gidion Paul (28) mkazi wa Igoma walikamatwa na
polisi eneo la Nyakato Sokoni Machi 2, mwaka huu majira ya 12:30 jioni wakisafirisha
mirungi kg 20 kwa kutumia pikipiki aina
ya HONLG yenye namba za usajili MC 931CKL.
Kwa mujibu wa Muliro polisi wanaendelea
na mahojiano dhidi ya watuhumiwa wote baada ya kukamilika kwa uchunguzi watafikishwa
mahakamani haraka iwezekanavyo na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano
kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa
katika vyombo sheria.
Pia amewaonya waendesha
pikipiki za bodaboda wanaojihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya kuwa
wanachafua taswira ya biashara yao na wasithubutu kujiingiza kwenye mfumo huo.
“Sheria inazuia kulima,
kusafirisha, kuuza na kutumia bangi na mirungi, ni makosa ya jinai vilevile Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mwanza linawataka askari wake kufanya kazi kwa weledi na
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi,”alisema Muliro.
Kamada wa Polisi mkoani Mwanza akionyesha gari lenye namba T 787 DQX
mali ya Peter Charles maarufu Peter Mirungi baada ya kulikamata likiwa
na kg 9.2 za dawa za kulevya aina ya mirungi.Picha na Baltazar Mashaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...