Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi amaliza rasmi ulaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya maafisa ardhi wa jiji la Arusha.
Waziri Lukuvi amesema hayo mkoani Arusha tarehe 8/3/2020 wakati wa ziara yake ya kuanzisha rasmi ofisi za ardhi za mikoa na kuvunja ofisi za kanda ambazo zilikuwa zinahudumia zaidi ya mkoa mmoja, hali iliyokuwa inawasababishia wananchi usumbufu.
Akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati akianzisha rasmi ofisi mpya ya kanda ya mkoa wa Arusha amesema kuanzia sasa ulaji uliokuwa unafanyika na baadhi ya maafisa aridhi wa jiji kwa kudai posho za kwenda kufuatilia hati mkoa wa kilimanjaro ameaumaliza rasmi.
Ameongeza kuwa Huduma zote za utoaji hati, uandaaji wa michoro ya mipango miji, pamoja na huduma za Msajili wa Hati zitatolewa Katika Jiji la Arusha na sio katika makao makuu ya kanda Moshi kama ilivyokuwa hapo awali.
Hadi sasa Waziri Lukuvi ameishafungua ofisi za ardhi ngazi ya mkoa katika mikoa ya Singida, Tabora, Geita, Mara na Arusha na kazi inaendelea katika mikoa mingine yote nchini ambapo huduma zote za uandaaji na utoaji hati kuanzia sasa zinafanyika mkoani.
Hatua hii ya kuanzisha ofisi za ardhi ngazi ya mkoa imekuja ili kupunguza kero za wananchi kufuata huduma hiyo Wizarani au katika Makao makuu ya Ofisi za Kanda za mikoa mitatumitatu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akizungumza na viongozi pamoja na maafisa wa mkoa wa Arusha wakati wa
kuanzisha rasmi ofisi ya ardhi ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha
Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akimsikiliza Mzee Mashauri Rajabu mkazi wa Arusha mwenye mgogoro wa
ardhi ambapo waziri Lukuvi alimueleza afikishe mgogoro wake katika ofisi
mpya ya Kamishna wa ardhi mkoa wa Arusha.
Viongozi na maafisa wa mkoa wa Arusha wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kuanzisha rasmi ofisi ya ardhi ya ka nda ya mkoa wa Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...