Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha (DVC(AF) Prof. Ernest Kihanga akitoa
ufafanuzi kwa Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, kuhusu maendeleo ya
ujenzi wa vyumba vya Madarasa, mradi mpya ambao unahusisha ujenzi wa vyumba vya
madarasa, kumbi za mikutano na ofisi za watumishi, eneo la Maekani Chuo Kikuu
Mzumbe.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha (DVC(AF) Prof. Ernest Kihanga akitoa maelezo kwa Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu
ujenzi wa Mabweni unaotarajiwa kumalizika kabla ya Juni 2020; wenye thamani ya
TSh. Bil 6.5 Maekani Kampasi Kuu.
Baadhi
ya Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwasili
eneo la Maekani kunakojengwa Hosteli za kisasa za Chuo Kikuu Mzumbe. Fedha za
Ujenzi zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Maafisa
Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha ya
pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha (DVC(AF) Prof. Ernest
Kihanga mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya kisasa Maekani,
mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Maafisa
Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakitembea kuelekea
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hosteli za kisasa Maekani Chuo Kikuu Mzumbe
Kampasi Kuu.
Maafisa
Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwa kwenye ofisi ya
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe walipowasili kutembelea maendeleo ya miradi
inayotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali. Maafisa hao wa Mkoani Morogoro
kushiriki kikao kazi kinacholenga kutangaza mafanikio ya Wizara.
====== ======== =======
Maafisa
Mawasiliano toka Taasisi na Vyuo Vikuu vya Umma vilivyopo chini ya Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia, wametembelea miradi ya maendeleo inayofadhiliwa
na Serikali ya Awamu ya Tano , Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha (DVC(AF) Prof.
Ernest Kihanga, akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema, mpaka sasa
maendeleo ya ujenzi wa mabweni unaendelea vema na unatarajiwa kukamilika mapema
mwezi Juni mwaka huu 2020.
“Tunashukuru
sana Serikali kuona umuhimu mkubwa wa kuwekeza kwenye ujenzi wa Mabweni,
tunaimani kubwa baada ya mradi huu kukamilika zaidi ya vijana 1000 watapata
malazi na hivyo tutadahili wanafunzi wengi zaidi wanaomaliza shule na kukosa
nafasi kwenye vyuo vyetu” alisema
Mbali
na mradi wa ujenzi wa mabweni, Chuo hicho kinaendelea na ujenzi wa vyumba vya
madarasa, kumbi za mikutano na ofisi za Watumishi ambapo kukamilika kwa jengo
hilo kutawezesha vijana zaidi ya 1000 kushiriki masomo kwa mara moja. Mradi huo
unakusudiwa kukamilika mwezi Juni 2020.
Mradi
wa Ujenzi wa mabweni unafadhili na Serikali ya Awamu ya Tano kwa Tshs. Bil 6.5
wakati ujenzi wa vyumba vya madarasa na kumbi za mikutano unategemea mapato ya
ndani na utagharimu takribani Tshs. Bil 3.5
Wakizungumza
mara baada ya ziara hiyo; maafisa hao wameonyesha kufurahishwa na uwekezaji
mkubwa unaofanywa na Serikali kupitia Taasisi zake, na kwamba hatua hiyo
itawezesha watanzania wengi kujiunga na Elimu ya juu nchini inayotolewa na Vyuo
vya Umma.
Maafisa
Mawasiliano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wako mkoani Morogoro
kushiriki kikao kazi kilicholenga kupanga mikakati ya uhamasishaji na Elimu kwa
Umma kuhusu shughuli zinazofanywa na kusimamiwa na Wizara hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...