Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu ya Jamii
MWANASIASA mkongwe nchini ambaye kwa sasa ni Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema anamshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kukutana na kufanya mazungumzo naye.

Maalim Seif amekutana na Rais Magufuli ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ajiunge na ACT –Wazalendo akitokea Chama cha Wananci(CUF).Hata hivyo kabla ya kuondoka CUF alishawahi kukutana na kufanya mazungumzo na Rais.

Akizungumza baada ya mazungumzo yake na Rais Magufuli, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa wamezungumza mambo mengi yanayohusu nchi yetu na kubwa zaidi ni kuendelea kudumisha amani, umoja,  mshikamano na kuendeleza upendo miongoni mwetu.

“Rais wetu ni muwazi na nimefurahi sana kukutana naye , amekuwa Rais anayependa kukutana na raia wake,  ndio maana leo nimekutana naye na tumezungumza mengi,”amesema Maalim Seif.
Alipoulizwa ni kitu ambacho wamezungumza na Rais Magufuli walipokutana, amejibu kuwa wamezungumza mambo mengi lakini yale ya ndani yatabaki kuwa ya kwake na Rais huku akisisitiza kufurahishwa na kukubaliwa na Rais kuzungumza naye. “Namshukuru Rais amekubali nikutane naye.”

Mbali ya Maalim Seif wengine ambao wamekutana na Rais leo Ikulu jijini Dar es Salaam ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF) Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.
   
Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo na viongozi hao, picha inayomuonesha akisalimiana na Maalim Seif kwa kugongesha miguu imekuwa gumzo kubwa mtaani na kwenye mitandao ya kijamii.Kwa kukumbusha tu kwa sasa nchi nyingi duniani ziko kwenye tahadhari ya ugonjwa Corona na njia moja wapo ya kuepuka ni kutopeana mikono.
Hivyo salamu ya Rais Magufuli na Maalim Seif kugongesha miguu wakati wakisalimiana inaonesha ishara ya wananchi kuchukua tahadhari hata kama ugonjwa huo haujafika nchini kwetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...