Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu Jamii
WAKAZI watatu wa jijini Dar es Salaam Jimmy Mlaki (23), mkazi wa Kinondoni Moscow, Stanley Ngowi maarufu kama Sultani (24), mkazi wa Tabata Segera na Issa Omari (29) wa Kimara wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon
amedai mbele ya Hakimu Mkazi Rashid Chaungu kuwa Januari 27 mwaka huu
huko Ubungo Kibo ndani ya wilayani Ubungo jijini Dar es salaam
washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine
zenye uzito wa gramu 509.63 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa na
kinyume cha sheria.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu ama kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 17, mwaka huu.

Wakati huo huo Fundi bomba Daniel Chizuwa mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kukutwa na kobe wawili kwenye thamani ya USD 140 ambazo ni sawa Sh. 320, 600 za kitanzania mali ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyamapori.
Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 22, mwaka 2020 huko maeneo ya Cliff Side jijini Dar es Salaam.
Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 22, mwaka 2020 huko maeneo ya Cliff Side jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...