Na Woinde Shizza,KARATU
MADEREVA bodaboda wametakiwa kujali mabinti, kwa kuwaacha wasome ili watimize ndoto zao na si kuwalaghai kwa kuwapa lifti pamoja na chipsi kwa wanapofanya hivyo wanawaharibia ndoto zao .
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo alipokuwa akihutubia katika mdahalo juu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika uwanja wa Mnadani wilayani Karatu,mdahalo ulioandaliwa Shirika la World Education Initiative (WEI) Bantwana; waache wasome ambalo lipo chini ya ufadhili wa watu wa marekani USAID.
Mahongo aliwasihi madereva bodaboda kuwa mfano katika wilaya ya Karatu kwa kuwatoa watoto sehemu husika kuwapeleka shuleni kama wakienda kuwachukuwa shuleni basi wawarudishe nyumbani wakiwa kwenye mikono salama na sio kuwarubini na kuwalaghai ili mradi wawachezee na wawakatishe masomo yao
Aidha alipongeza shirika la (WEI) kwa kuandaa mdahalo huo na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wanaojihusisha na shughuli za bodaboda kwa kazi ya kubeba vijana na kupeleka shuleni.
Alibainisha kuwa wanawake wote wanatambuliwa duniani, ndio maana Tanzania Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuliona hilo alimchagua msaidizi wake ambaye ni makamu wa Rais kuwa mwanamke.
“Mzazi anamuandaa binti yake kuwa mfanyakazi au kiongozi ili baadae aje kusaida familia, anapokumbwa na watu wanao mlaghai, binti zile ndoto zake zinayeyuka,binti anakuwa bado ni mtoto na anapata mtoto katika umri mdogo na anakuwa ni mzigo kwa mzazi, " Mahongo
Mahongo amewaomba wananchi wa Karatu kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa korona, kwa kuepuka kupeana mikono. Amesema ugonjwa huu umesambaa kwa nchi takribani 84 duniani kwa sasa, ameomba wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa idara ya afya. Amesema wilaya ya Karatu imeshajiandaa kukabiliana na ugonjwa huo lakini bado amehimiza wananchi kuchukua tahadhari kubwa juu ya ugonjwa huo.
Mtaalamu wa jenda na jinsia katika shirika la (WEI) ambalo liko chini ya udhamini wa watu wa marekani Grace Muro amesema wamejikita katika kufanya kazi katika shule za sekondari za kutwa mbazo zimekuwa na tatizo kubwa la watoto wa kike kukatishwa masomo yao kwa sababu ya mimba.
Alisema wao kama (WEI) wamekuja kufanya kampeni ili jamii iweze kuwa na uelewa juu ya athari za mimba za utotoni, amesema hawa watoto wa kike ni wakinamama tunaotarajia kuleta maendeleo siku za usoni, Lazima tuhamasishe jamii kuacha mila potofu zinazofanya mtoto kike kuwa duni, tumelenga kampeni yetu kwa hawa madereva wa bodaboda ambao kidole kinalenga kwao waweze kuchangia maendeleo ya mtoto wa kike aliwaomba madereva bodaboda kuwaona watoto wa kike kama dada zao, na wajikite katika shughuli za kujipatia kipato.
John Lucian Katibu wa madereva bodaboda wa zamani alisema ni lazima watoto wa kike nao wawe na maadili lakini amesisitiza kuongeza elimu ya madili kwa wazazi.
Alisema ni lazima wazazi wajenge mabweni ili wanafunzi wa kike wawe shuleni au wajenge shule za sekondari karibu na maeneo ambayo ni rafiki kwa wanafunzi kike ili wanaweza kufika kwa urahisi shuleni.
Aidha alisema kuna tatizo la mimba kwa watoto wa kike ambalo linamalizwa kinyumbani jambo ambalo linafanya kesi za mimba kuendelea kuongezeka na kuwataka wanaohusika na utetezi wa haki za kisheria za watoto wa kike kupata mimba mashuleni, kuongeza umakini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...