Hali ya taharuki imetanda nchini Zimbabwe baada ya mtu anayeshukiwa kuwa na virusi vya Corona kutoroka hospitalini alikokuwa amewekwa karantini na kwenda kusikojulikana.
Gazeti la serikali la Herald limeripoti kuwa, mshukiwa huyo wa Corona alikuwa ametengwa katika chumba maalumu akisubiri kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Wilkins katika mji mkuu Harare kabla ya kukimbia.
Vyombo vya dola nchini humo vimesema vimeanzisha msako mkali wa kumtafuta raia huyo wa Thailand, anayeshukuwa kuwa na virusi vya Corona.
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika haina kesi ya Corona iliyothibitishwa kufikia sasa, lakini katika nchi jirani ya Afrika Kusini, kesi saba za ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi hivyo zilikuwa zimenakiliwa kufikia jana.
Katika hatua nyingine, Burkina Faso ndiyo nchi ya hivi punde ya chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuripoti kesi ya Corona. Katika kikao na waandishi wa habari mjini Ougadougou hapo jana, Waziri wa Afya, Claudine Lougue amesema watu wawili (mme na mke) wamewekwa chini ya karantini baada ya kurejea nchini humo wakitokea Ufaransa.
Burkina Faso ni katika nchi chache za chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuripoti kesi za Corona; nchi zingine zikiwa ni Senegal, Afrika Kusini, na Nigeria. Nchi kadhaa za kaskazini mwa Afrika kama Tunisia, Algeria, Morocco na Misri zimeripoti visa kadhaa vya ugonjwa huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...