Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwani, imemuhukumu aliyekuwa meneja wa
kituo cha kuuza mafuta cha UKODI INTERNATIONAL COM LIMITED, Malima
Charles miaka 40 mkazi wa Maili moja Kibaha, kwenda jela miaka mitano
baada ya kumkuta na hatia katika makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili
ikiwemo kuvunja ofisi na wizi.
Akisoma
hukumu hiyo iliyodumu kwa muda wa saa moja ambayo ilivuta hisia za
wakazi wa Kibaha, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Joyce Mushi, alieleza
kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri .
Pia
kuwa fundisho kwa watumishi wengine wanaopewa dhamana ya kusimamia
vituo vya mafuta hivyo mahakama imemkuta na hatia na kumhukumu kwenda
Jela miaka 5 kwa makosa yote mawili
Mwendesha
mashtaka katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali Auleilia Mushi alieleza
mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa akiwa meneja wa kituo cha kuuza mafuta cha
UKODI INTERNATIONAL COM LIMITED, alikula njama za kuvunja ofisi na kuiba
kiasi cha fedha za Kitanzania zipatazo milioni 45,26613 za mwajiri wake
na kutoweka kusikojulikana huku akijua fika kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Mwendesha
mashitaka huyo wa Serikali aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alivunja ofisi
hizo tarehe 24.12.2018 na kuondoka na mauzo ya siku husika ambayo
yalikuwa hayajapelekwa kuhifadhiwa Bank kutokana na siku hiyo kuwa ni
siku ya mwisho wa juma na baada ya kutekeleza wizi wake akatoweka hadi
pale jitihada zilipofanyika za Jeshi la Polisi kuweza kumsaka na kumtia
nguvuni na kuweza kufikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa hatua za
kisheria.
Akijitetea
mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo mtuhumiwa huyo Malima Charles
maarufu kwa jina la Mukama alikiri kufanya kosa hilo na kuiomba mahakama
hiyo impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na ana familia
inayomtegemea na yeye akiwa ana matatizo ya kiafya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...