Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk.
Titus Kamani akizungumza na Wakulima wa zao la Choroko na wanachama wa
Vyama vya Msingi vya Ushirika wakati akizindua Mnada wa zao la Choroko
kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” katika moja ya Ghala kwenye
kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
leo Jumatano Machi 11,2020. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akizungumza
na Wakulima wa zao la Choroko na wanachama wa Vyama vya Msingi vya
Ushirika wakati akizindua Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao
“Online Trading System”.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa, Augustino
Mbulumi akionesha matokeo ya mnada wa leo Machi 11,2020 jumla ya kilo
2000 za choroko zimeuzwa kwa bei ya shilingi 1340 kwa kilo moja.
Katika mnada wa leo Machi 11,2020 wanunuzi wawili
walijitokeza kununua choroko kiasi cha kilo 2000 ambapo mnunuzi wa
kwanza alitoa bei ya shilingi 1340 na mnunuzi wa pili alitoa shilingi
1,248 kwa kilo moja kununua kilo 2000 za choroko.
Naibu Mrajis wa Vyama Vya
Ushirika Tanzania, Charles Malunde akizungumza wakati wa uzinduzi Mnada
wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ambapo
alisema serikali itahakikisha mazao yote yanaingia katika mfumo wa
Stakabadhi ghalani ili wakulima wanufaike kupitia kilimo.
Kaimu Mrajis Msaidizi Tume
ya Maendeleo ya Ushirika, Benjamini Mwangala akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Mnada kwa Mfumo wa Mtandao kwa ajili ya zao la Choroko.
Alisema uzinduzi huo waMnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao
“Online Trading System” ni sehemu ya utekelezaji wa Tangazo la Waziri wa
Kilimo alilolitoa Februari 14,2020 kuzindua Mnada wa Soko la Bidhaa kwa
mazao ya jamii ya mikunde na mbegu.
Sehemu ya choroko ikiwa kwenye magunia katika ghala la kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali.
Katikati ni Meneja wa Chama
Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), Ramadhani Kato
akizungumza na Mkulima wa choroko Kwiyolecha Nkilijiwa. Kulia ni
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo
ya Ushirika Tanzania (Tanzania Cooperative Development Commission -TCDC )
Dk. Titus Kamani amezindua Rasmi Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa
Mtandao “Online Trading System” katika Mkoa wa Shinyanga na Mwanza.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Machi 11,2020 katika kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Dk. Kamani alisema lengo la
serikali ni kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao na kuuza mazao yao
kwa bei nzuri hivyo anaamini Mnada wa Choroko kwa kutumia mfumo wa
mtandaoni utasaidia wakulima kuuza mazao kwa bei ya juu.
“Wakulima mlikuwa mnauza
choroko kwa bei ya chini inayoumiza,vitini vya choroko vilikuwa
vinachezewa. Na sasa ili kupata bei nzuri ni kwenda mnadani ambapo
kutakuwa na bei ya ushindani na ukiridhika na bei ndiyo unauza na kupewa
fedha zako”,alisema Dk. Kamani.
“Hamasisheni wakulima
wajiunge kwenye Vyama vya Msingi ‘AMCOS’ ,kwani mnada utafanyika kupitia
AMCOS ambapo kila mkulima atapeleka choroko yake na kuangalia bei ya
ushindani itakayokuwepo siku ya mnada na atalipwa fedha zake ndani ya
saa 72”,aliongeza Dk. Kamani.
Aidha alisema mbali na Mnada kwa
mfumo wa Mtandao kumnufaisha mkulima pia utasaidia Chama Kikuu Cha
Ushirika na Halmashauri za wilaya kupata fedha huku akisisitiza kuwa bei
ya ushindani inakwenda kwa mkulima bila makato.
Kwa upande wake, Kaimu Mrajis
Msaidizi Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Benjamini Mwangala alisema
uzinduzi huo wa Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ni
sehemu ya utekelezaji wa Tangazo la Waziri wa Kilimo alilolitoa
Februari 14,2020 kuzindua Mnada wa Soko la Bidhaa kwa mazao ya jamii ya
mikunde na mbegu.
“Tangazo hilo linataka mazao
ya Jamii ya Mikunde na mbegu kama vile mbaazi,choroko,dengu,ufuta na
soya kuuzwa kupitia Vyama vya Ushirika ili mkulima apate bei nzuri na ya
ushindani mahali alipo”,alisema Mangwala.
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Soko la Bidhaa, Augustino Mbulumi alisema katika mnada wa leo Machi
11,2020 jumla ya kilo 2000 za choroko zimeuzwa kwa bei ya shilingi 1340
kwa kilo moja.
Aliwasihi wakulima wajikusanye
wapeleke mazao yao katika AMCOS na kukusanya mazao mengi ili kuvutia
wanunuzi wakubwa wenye bei nzuri ili mkulima anufaike kupitia zao hilo
la choroko.
Naibu Mrajis wa Vyama Vya
Ushirika Tanzania, Charles Malunde alisema serikali itahakikisha mazao
yote yanaingia katika mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo mnada utakuwa
unafanyika kupitia mtandao ili wakulima wanufaike kupitia kilimo.
Mkulima wa choroko Kwiyolecha
Nkilijiwa aliiupongeza serikali kwa kuanzisha mnada wa mazao akieleza
kuwa wakulima walikuwa wanapata hasara kutokana na kuuza choroko yao kwa
bei ya chini ambapo hapakuwa na vipimo walanguzi walikuwa wananunua kwa
Rumbesa/visado kuanzia shilingi 600 hadi 1000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...