Mhandisi wa ujenzi wa Jengo la
Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani Suleiman Nassor
akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na
Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhusu
Jengo hilo litakavyokuwa wakati Makamu wa Rais alipotembelea
kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo leo March 14,2020 Kibaha
Mjini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam
na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi, Wanachama wa Chama
cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwenye Harambee ya Ujenzi wa
Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani
iliyofanyika leo March 14,2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha
Mjini. Jumla ya Shilingi Milioni 584 zimechangishwa ikiwemo ahadi ya Mifuko 400 ya Saruji na Ndoo 50 zimechangishwa kwa ajili ya
kukamilisha Ujenzi huo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe.
Jakaya Kikwete akizungumza kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi
na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyoongozwa na Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa
wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Ukumbi wa Chuo cha
Uuguzi Kibaha Mjini leo March 2020.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam
na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi,
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa wa Pwani mara
baada ya kuongoza Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la
Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyofanyika leo March 14,2020 katika
Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Mjini. Jumla ya Shilingi Milioni 584 zimechangishwa ikiwemo ahadi ya Mifuko 400 ya Saruji na Ndoo 50 zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam
na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana kwa Ishara na Viongozi wa Mkoa wa
Pwani alipowasili katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Pwani Leo
March 14,2020 kwa ajili ya kuongoza Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi
na ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani. Jumla ya Shilingi
Milioni 584 zimechangishwa ikiwemo ahadi ya Mifuko 400 ya Saruji na Ndoo
50. zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam
na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza Jambo kwa Viongozi wa Mkoa wa
Pwani kuhusu Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM
Mkoa wa Pwani alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo
Kibaha Mjini leo March 14,2020.kulia ni Rais Mstaafu awamu ya Nne Mhe.
Jakaya Kikwete.
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Ali
Makoa akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
kuhusu litakavyokuwa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM
Mkoa wa Pwani litakapokamilika alipotembelea kuangalia Maendeleo ya
Ujenzi wa Jengo hilo leo March 14,2020 Kibaha Mjini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani
Ramadhani Maneno akimkabidhi Tuzo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani
ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye Harambee
ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi la CCM Mkoa wa
Pwani uliofanyika leo March 14,2020 Kibaha Mjini.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...