Na Luteni  Selemani Semunyu

Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete amewataka wanawake nchi kusimama imara katika kujiendeleza katika nyanja mbali mbali ikiwemo michezo na kuliletea Taifa heshima bila kujali tofauti za jinsi walizonazo.

Aliyasema hayo wakati akifunga Mashindano ya kuadhimisha siku ya mwanamke duniani kwa mchezo wa Gofu katika yaliyofanyika Jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Mama Salama alisema  licha ya michezo mingi kuonekana kuchezwa na wanaume na wanawake kuingia katika michezo hiyo sasa ni wakati kwa wanaume kucheza michezo iliyokuwa ainaonekana kama ya wanawake kama mpira wa pete.

” Kama tatizo ni Mavazi basi zitafutwa nguo za aina  Nyingine zitakazotumika katika mchezo huo ili kuhakikisha wanashiriki wanaume kama ambavyo wanawake wanashiriki. “ Alisema Mama Salma Kikwete.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema   anajivunia mafanikio makubwa ya Klabu ya Lugalo kwa mafanikio makubwa yaliyoletwa na wanawake kutokana na kuleta Vikombe ndani na Nje .

“ Kiukweli tangu nimekuwa Mwenyekiti wa Lugalo sijawahi kupata kikombe kutoka kwa wanaume hasa ya Nje ya Nchi  lakini Wanawake wamekuwa wakinitoa kimasomaso  na najivunia na imekuwa changamoto kwa Wanaume katika kufanya Vizuri, Alisema Mwenyekiti Lugalo.

Kwa upande wake Nahodha wa Wanawake wa Lugalo Hawa Wanyenche alimuomba Mama Salma kuwa Mlezi wa Timu ya Wanawake na kuweza kusaidia ikiwemo Timu ya Taifa ya Wanawake.

Kwa upande wa Matokeo ya Mashindano hayo Mchezaji Angel Eaton alifanikiwa kuibuka Mshindi wa Jumla baada ya kupata Mikwaju  80  huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tatu  huku katika  Fedha  Mshindi ni Salma Juma akifuatiwa na Amina Hamisi.

Wakati katika Shaba  Mshindi ni Christina Charles aliyepata Net ya 74  huku katika kundi la Wanawake wenye umri Mkubwa  Ladies Senior Mshindi ni  Stephani Sayore.
 Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu ya wanawake ya Lugalo katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
 Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Watoto waliopata Zawadi katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
 Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji mbalimbali mara baada ya  kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...