Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakiwa kwenye maandamano kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo Kimkoa wa Dodoma yamefanyika katika Shule ya Msingi ya Mkonze jijini Dodoma.
Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la Umeme nchini Tanesco wakiwa kwenye picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo mkoani Dodoma yamefanyika jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Amani jijini Dodoma wakiwa kwenye maandamano katika viwanja vya Mkonze katika siku ya wanawake duniani ambapo maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika jijini Dodoma.
Wanawake mbalimbali waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo mkoani Dodoma yamefanyika katika Shule ya Msingi Mkonze wilayani Dodoma.

Charles James, Globu ya Jamii
WANAWAKE wametakiwa kujiamini kuwa wanaweza na kukimbilia fursa mbalimbali za kimaendeleo kwani jambo lolote analoweza kufanya mwanaume hata wao wanaweza.

Kauli hiyo imetolewa na Injinia Sophia Mgonja ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umeme (Tanesco) katika maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Mkonze iliyopo jijini Dodoma.

Injinia Mgonja amesema wanawake hawapaswi kuwa wanyonge kwani kwa miaka ya hivi karibuni wamefanya mambo makubwa ambayo yamekua yakifanywa na wanaume.

"Wanawake tujiamini tuna nafasi kubwa sana kama tutaamua kuacha uoga na kukimbilia fursa, leo hii Naibu Spika wa Bunge ni mwanamke Dk Tulia Ackson lakini pia tuna Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Tusiogope sisi ni Jeshi kubwa tunaweza." Amesema Injinia Mgonja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyakazi Wanawake wa Tanesco, Renilda Kageuka amesema usawa katika nafasi za kimaamuzi uwepo ili kuakisi kauli mbiu ya mwaka huu isemayo ' Kizazi cha usawa kwa maendeleo ya sasa na baadae'.

Amewataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu jambo ambalo litawafanya wazidi kuikaribia 50 kwa 50 katika ngazi za kiuongozi.

" Muamko kwa sasa ni mkubwa hata kwa wazazi katika kuwapa elimu na kipaumbele watoto wa kike hili limefanya leo tuwe na idadi kubwa ya wasomi wanawake," Amesema Renilda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...