Marekani
imeeleza kufurahishwa na mafanikio ya Tanzania katika masuala ya
ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za uongozi wa kisiasa na maamuzi
na hatua zilizochukuliwa kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata
elimu bora na salama.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na mshauri wa Rais Trump kuhusu masuala ya maendeleo
ya wanawake Balozi Kelley Currie mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi
za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Washington.
Mara
baada ya kukutana na mshauri huyo wa Rais Trump kuhusu masuala ya
maendeleo ya wanawake Balozi Kelley Currie Prof. Kabudi pia amekutana na
kufanya mazungumzo na kundi la Washington Intergovermental
Professionals Group wakiwemo maseneta na mabalozi kutoka nchi mbalimbali
waliopo Marekani kwa lengo la kuwaelezea fursa za uwekezaji zilizopo
nchini.
Balozi
wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Willson Masilingi kwa upande wake
amesema ziara ya Prof. Kabudi nchini Marekani kwa kiasi kikubwa
imesaidia kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Marekani
na kwamba nafasi ya kukutana na makundi mbalimbali yatahamasisha
wawekezaji wengi marekani kwenda Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...