Watumishi wa mamlaka ya
Wanyamapori TAWA Mkoa wa Morogoro wakiwa katika maanadamano,katika siku
ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Watumishi wa mamlaka ya
Wanyamapori TAWA Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wakiadhimisha siku ya wanawake duniani katika Halmashauri ya Manispaa
ya Morogoro.
………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY MOROGORO.
Wakati dunia inaadhimisha siku ya
mwanawake duniani wanawake nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele
katika mapambano dhidi ya majangili ili kulinda nyala za serikali
hususani wanyama pori.
Wito huo umetolewa katika kilele
cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,Manispaa ya Morogoro na Bi
Cassia Mayombo kutoka kitengo cha utawala mamlaka ya wanyama Pori (TAWA )
alikupokuwa anaongea na Fullshangwe Blog,ambapo amesema kuwa wao kama
TAWA wanatambua mchango wa mwanamke katika kupambana na majangili.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi
Mwandamizi Mahusiano kwa Umma mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA) Bwana Twah
Twahibu amesema kuwa askari wanawake wa wanyamapori(JESHI USU) wapo
vizuri katika kupambana na majangili wawapo porini hivyo amewataka
kuongeza kasi zaidi katika kazi yao.
Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo
ipo katika mchakato wa kufungua mabucha na mashamba ya kufugia
wanyamapori,hivyo wamewataka wadau mbalimbali kujitokeza kuomba nafasi
hizo zitakazokuza kipato chao na taifa kwa ujumla..
Katika hatua nyingine amewataka
wananchi hususani wa mkoa wa morogoro kutumia njia mbadala ya kuwafukuza
tembo wanaoingia katika mashamba yao kwakuweka mizinga ya nyuki jambo
litakalowasaidia kuepukana na wanyama hao kipindi mamlaka ikiwa
inaagalia namna ya kukabiliana na wanyama hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...