Na Said Mwishehe,Michuzi Blog ya jamii
MAWAZIRI wa sekta ya afya kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Nchi za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika( SADC) wamekutana jijini Dar es Salaam huku ajenda kuu kwa siku ya leo Machi 9 mwaka 2020 ikiwa ni kujadili mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona duniani.
Ugonjwa huo ambao uligundulika mwaka jana nchini China katika Jiji la Wuhan lililopo Jimbo la Hubei na kupewa jina la COVID-19, hadi kufikia jana umeshaua zaidi ya watu 3,800 duniani huku 100,008 wakiwa wakiambukizwa.
Tayari ugonjwa huo ambao umeshaathiri nchi za Italy, Iran, Korea Kusini, umeshasambaa katika baadhi ya nchi za Afrika zikiwamo Misri, Nigeria, Afrika Kusini, Algeria, Cameroon, pamoja na Togo na kwamba vifo kadhaa vimesharipotiwa.
Nchi nyingi duniani zimeanza kuchukua tahadhari katika mipaka yake ikiwamo viwanja vya ndege kwa kuweka vipimo vya kuwapima abiria wanaoingia katika nchi zao.
Hivyo mawaziri wa afya wa SADC leo 'walijifungia' kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni wakiongozwa na mwenyeji wao, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na kwamba walijadiliana namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...