Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Hadija Mwinuka ametoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum wawapeleke shule badala ya kukaa nao nyumbani na kuwafungia
Ameyasema hayo wakati akitoa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na wanawake viongozi wa Elimu Wilaya ya Tandahimba kwenye shule maalum mjimpya
Mwinuka ameeleza kuwa shule hiyo ni bweni hivyo wanapokea watoto wakike na wakiume wananchi waache kuwafungia ndani badala yake wawapeleke wakapate elimu mbalimbali katika shule hiyo
"Wananchi tuitumie shule maalum mjimpya kwa kuwapeleka watoto,walimu tunao wenye wito hivyo wanafundisha hadi mtoto anafika hatua ya kujihudumia yeye mwenyewe,tukiwaacha majumbani wqnaopata tabu ni akina mama,"amesema Mwinuka
Naye mwalimu Mkuu wa shule Mohamed chipuputa ameeleza kuwa wanafunzi hao wanafundishwa pia stadi za kazi wanapofikia hatua ya kujielewa hivyo inampa uwezo wa kupata kipato
"Tunawafundisha waweze kujihudumia wenyewe hapa tunawafundisha kuanzia watoto wa awali na kuendelea sambamba na shughuli za ufundi kama kushona,ufundi selemala,ufugaji na shughuli zingine ambazo hata akiwa nyumbani atasaidia kazi mbalimbali,"amesema Chipuputa

Kaimu Mkurugenzi Hadija Mwinuka akishiriki michezo na watoto wenye mahitaji maalum
Watoto wakipangwa kwa ajili ya michezo mbalimbali
Kaimu Mkurugenzi Hadija Mwinuka akitoa neno kwa wageni waalikwa
Walimu pia walishiriki michezo na watoto hao
Kaimu Mkurugenzi akikabidhi mwanagunzi msumeno utakaomwezesha katika shughuli zao za ufundi
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa watoto hao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...