Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho utaofanyika Mei 9 mwaka huu Kitapitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa jina Mgombea Urais lilisgapitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.
Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyopo amekidhi mahitaji ya watanzania.
"Hivi unasimamishaje Mgombea wakati Kazi aliyoifanya Rais aliyopo madarakani inaonekana, kungewepo na tatizo ndio kungekuwepo umuhimu wa kusimamisha mgombea"amesema Mrema
Aidha Mrema amemshauri Mwenyekiti wa chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia kuutangazia umma kuwa Uchaguzi Mkuu utakuwa wa Uhuru na Haki pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais aliopo madarakani.
Amesema Mbatia alishawahi kusema kuwa kusifu serikali ya iliyopo madarakani sio dhambi hivyo anaweza kuendelea kuunga mkono Rais wa Awamu ya Tano kuendelea kwa kipindi kingine.
Mrema amesema Rais Dkt.John Magufuli aachwe amalize malengo yake kuifikisha Tanzania anayoitaka ambayo ni Tanzania ya Maendeleo yanayoonekana.
Amesema TLP si chama cha kufuata upepo wa bendera bali ni chama kinachojua kinachofanyika na kuukubali uongozi ws Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Amesema vyama vingine vijifunze na kuangalia Rais Dkt.John Magufuli namna Tanzania iliyopata Maendeleo kw kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP, Mh. Agustino Latonga Mrema akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo kwenye makao Makuu ya
Ofisi hizo Magomeni jijini Dar kuhusu Mkutano
wao mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 9 mwaka huu na kwamba Kitapitisha Mgombea wa
Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP,Richard Lymo akizungumza jambo
mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo kwenye makao Makuu ya
Ofisi hizo Magomeni jijini Dar kuhusu Mkutano
wao mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 9 mwaka huu na kwamba Kitapitisha Mgombea wa
Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli. Pichana Michuzi JR-Michuzi Media.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...