Na Mwashungi Tahir Maelezo
Imeelezwa kwamba mfumko wa bei kwa mwaka uloishia February 2020 imeongezeka kufikia asilimia 6.2 ukilinganisha kwa mwaka ulioishia January 2020 asilimia 4.9
Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha mfumko wa bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abrahmani Msham wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ilioko Mazizini .
Amesema ongezeko hilo limetokana na bidhaa mbali mbali zikiwemo vyakula vilivyoongezeka Mchele wa Mbeya , Unga wa Sembe , mafuta ya dizeli. bidhaa zisizo kuwa na kilevi na bidhaa nyengine Unga wa Ngano .Samaki Ndizi Mbichi Sukari Nyeupe Ndizi mbivu na Saruji .
Nae Meneja Uchumi wa Bank KuuTawi la Zanzibar Moto Ng’wingamele Lugobi amesema bei imeongezeka lakini bado upo kwa lengo la Serikali ambapo mvua zikienda vizuri bei zitapungua.
Aidha aliwataka kuondosha wasi wasi kuhusu ongezeko la bei kwani hilo ni ongezeko la kawaida na mvua zikiwa zitakwisha bidhaa zitashuka.
Kwa upande wake Dr Esklla Ngoma Hassan Mchumi mwandamizi SUZA amesema kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ndio bei za bidhaa zinapanda ukilinganisha na Nchi nyengine za jirani ikiwemo Uganda.
Vile vile wananchi wamesema hivi sasa hali ya bei imezidi kuwa kubwa hali ambayo inawasababishia kutoweza kumudu kupata mahitaji ya lazima ikiwemo samaki, nyama bidhaa za nafaka, na baadhi ya bidhaa nyengine na misha yanazidi kupanda.

Mkuu wa Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis
Abdul-rahman Msham akitoa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kupanda kutoka
Asilimia 4.9 kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020
hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar.
Meneja Uchumi Benki kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele
Lugobi akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika hafla ya
utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kupanda kutoka Asilimia 4.9
kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020 hafla
iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar.
Mchumi mwandamizi Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk,Estella Ngoma Hassan akijibu maswali yalioulizwa atika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kupanda kutoka Asilimia 4.9 kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020 hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA /HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...