Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezuia uingiaji wa ndege za kitalii kutoka nchini Italy kuja Zanzibar ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa maradhi ya Corona.
Akizungumza na waandishi wa Habari Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja kuhusu mwenendo wa maradhi ya Corona yaliyosambaa Ulimwenguni amesema wamezuia uingiaji wa ndege hizo ili kuchukua tahadhari na ugonjwa huo usisambae nchini.
Alifahamisha kuwa hadi sasa zaidi ya nchi 85 za Umoja wa Mataifa zimeshaathirika na Virusi vya ugonjwa huo hivyo jamii inapasa kuchukua tahadhari kujikinga na kuwa makini na usambazaji.
Waziri Hamadi aliwataka wananchi kuchukuwa tahadhari kuhakikisha wageni wote wanaowasili nchini kufuata taratibu na masharti yaliyowekwa ili kuweza kudhibiti na kuepuka kusambaa nchini.
Waziri huyo wa Afya alisistiza kusitishwa shughuli zote ambazo zinahusisha mkusanyiko wa wageni kutoka nje ya nchi pamoja na wananchi kusafiri katika nchi ziliathirika na ugonjwa huo kwa lengo kulinda usalama wa maambukizi.
Hata hivyo alikemea tabia ya baadhi ya wananchi kuvumisha habari zisizo sahihi kutokana na maradhi hayo, hivyo ameitaka jamii kusikliza taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari ili kujua maendeleo na uhakika wa taarifa hizo kwa lengo la kuwaondolea hofu.
“Zanzibar ugonjwa huu bado haujaingia ila wananchi wawe na tahadhari maalum ili kujikinga”, alieleza Waziri Hamad.
Alifahamisha kuwa serikali tayari inachukua tahadhari kwa kuweka mfumo wa kinga wa udhibiti katika Viwanja vya Ndege na maeneo ya Bandari wananchi wanaoingia nchini wanafanyiwa vipimo pamoja na kuundwa timu pamoja kutenga eneo maalum katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja na Kidimni kwa ajili ya wagonjwa na watakaogundulika na ugonjwa huo .
Aidha Waziri Hamad aliipongeza Ofisi ya Mufti kwa kuzuia Ijitimai ya Kitaifa iliyotarajia kufanyika nchini pamoja na sherehe za wageni (Fullmoon Part) kwa wageni kwa lengo la kuchukua tahadhari ya maradhi ya Corona
Nae Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk Fadhil Mohamed Abdalla aliwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kufanya usafi kwa kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kutia mkono, machoni, mdomoni na puani ili kujikinga na ugonjwa huo.
Mkurugenzi huyo alifahamisha dalili za maradhi ya corona ni kuwa na homa kali, mafua makali na joto kubwa mwilini pamoja na kutoweza kupumua hivyo jamii iendelee kudumisha usafi kwani ndio silaha ya afya.

Waziri wa Afya Hamad Rashid akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana
na Maradhi ya Korona yalioingia katika baadhi ya Nchi Duniani ambapo
hadi sasa Zanzibar na Tanzania kwa Jumla hakuna maradhi hayo na kuelezea
Tahadhari za kujikinga zilizochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na
madawa na Vifaa vya kujikingia hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara hio
Mnazi mmoja Zanzibar.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk Fadhil Mohamed Abdalla akijibu
baadhi ya maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na
Maradhi ya Korona yalioingia katika baadhi ya Nchi Duniani ambapo hadi
sasa Zanzibar na Tanzania kwa Jumla hakuna maradhi hayo na kuelezea
Tahadhari za kujikinga zilizochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na
madawa na Vifaa vya kujikingia hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara hio
Mnazi mmoja Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Afya Hamad Rashid kuzungumzia Maradhi ya Korona yalioingia katika baadhi ya Nchi Duniani ambapo hadi sasa Zanzibar na Tanzania kwa Jumla hakuna maradhi hayo na kuelezea Tahadhari za kujikinga zilizochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na madawa na Vifaa vya kujikingia hafla iliofanyika ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...