Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

TAKWIMU za maambukizi ya Ukimwi nchini Tanzania kwa sasa yanayonesha kuwa kwa mwaka kuna maambukizi mapya 72000 na kwa siku kuna maambukizi mapya ya watu 200 na hivyo kufanya kila saa moja kati ya watu nane hadi tisa wanaambukizwa ugonjwa huo.

Akizungumza leo Machi 6 mwaka 2020 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) Dk.Leonard Maboko amefafanua mwaka 2016 hadi mwaka 2017 ulifanyika utafiti na kubaini kwa mwaka kuna maambukizi mapya ya Ukimwi 72000, watu 6000 kwa mwezi, watu 200 kwa siku na kwa saa watu nane au tisa wanaambukizwa ugonjwa huo.

"Katika maambukizi hayo mapya inaonesha asilimia 40 wanaopata maambukizi ni vijana na hilo ni kundi kubwa ambalo ni nguvu kazi ya Taifa letu.Hivyo moja ya mkakati ambao tumekuwa nao ni kutumia majukwaa ya vijana kuhakikisha tunatoa elimu ambayo itasaidia kupunguza kasi ya maambukizi kwa vijana nchini.

"Kuwepo kwa maambukizi kwa vijana walio wengi TACAIDS tuliamua kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi katika makundi mbalimbali na mwaka 2019 tuliamua kushirikiana na Bongo Star Seach(BSS) kwa kutumia jukwaa lao la wasanii na shughuli nyingine wanazozifanya kwa kuamini hiyo ni sehemu sahihi ya kuendelea kutoa elimu hiyo,"amesema Dk.Maboko.

Ameongeza kutokana na takwimu hizo Waziri Mkuu alishatoa maagizo kwamba wafanye kazi na vijana na hivyo wamekuwa wakijihusisha na makundi mbalimbali ya vijana kwa kuwapatia elimu ambayo itawezesha vijana kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo.

"Jukwaa la BSS limetoa fursa nzuri kwetu kufikia vijana wengi na kuwapatia elimu hii.Tukiwa kwenye majukwaa ya BSS watu wetu wa TACAIDS walikuwepo. Hivyo mbali ya kutoa elimu watu walipima kufahamu kama wanaambukizi , tuligawa kondomu na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo,"amesema.

Dk.Maboko amesema  Star Times na BSS ni watu wema , hivyo waliamua kuhamasisha jamii  kupitia majukwaa hayo kwa kuanzisha mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajili ya wanaotoa elimu ya uhamasishaji kujikinga na ugonjwa huo kwa kutumia namba za simu 0684 909090 na hilo limeleta mafanikio makubwa na kufafanua asilimia tano ya fedh hizo zimetolewa kwa mfuko huo.Pia amesema TACAIDS waliamua kuwapa elimu walimu 300 kuhusu namna bora ya kufundisha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi ambao nao wamekuwa wakienda kuhamasisha jamii kujiepusha na ugonjwa huo.

Amefafanua wameanza kutoa elimu hiyo jijini Dar es Salaam na wataendelea na mikoa mingine na bahati nzuri Wizara ya Elimu inayo mitaala mizuri ambayo imekuwa ikitumika kwenye kuifundisha jamii kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo na elimu ya uzazi kwa ujumla na hasa inayolenga kujitambua.

Hata hivyo amesema huko nyuma kulikuwa na matangazo mengi yanayohusu Ukimwi na kuna kila sababu ya kuongeza kasi ya utoaji elimu kuhusu ugonjwa huo na utafiti unaonesha kwamba chini ya asilimia 50 ndio inafahamu kuhusu uelewa wa Ukimwi na hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kutolewa elimu hiyo na hakuna sababu ya kulega lega.
Mwakilishi wa uongozi wa Bongo Star Search Bi. Eveline Byaruhanga (kushoto) akimkabidhi Dkt. Leonard Maboko (kulia) mchango wa fedha kwa lengo la kutunisha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) uliotolewa na uongozi huo. 

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) Dk.Leonard Maboko (katikati) akizungumza wakati wa kupokea fedha kutoka kwa uongozi wa Bongo Star Search BSS kwa lengo LA kutunisha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI. (ATF). Kushoto ni Mwakilishi wa uongozi wa BSS Bi. Eveline Byaruhanga na kulia ni Mwakilishi wa Startimes Ndugu. Fanny Kalinga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...