Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Daniel Shonza mapema leo akiwa na
mtoto mwenye ulemavu Mary Mwakanyamale ambaye amempatia kiti maalumu cha
watu wenye Ulemavu, Naibu Waziri Shonza ametoa vifaa mbalimbali vya
michezo, Elimu na Walemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 10,325,000
kwa Mkoa wa Songwe.

Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Daniel Shonza mapema leo akimkabidhi
Kompyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowo Grace Kashililika, Naibu
Waziri Shonza ametoa vifaa mbalimbali vya michezo, Elimu na Walemavu
vyenye thamani ya shilingi milioni 10,325,000 kwa Mkoa wa Songwe.

Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Daniel Shonza mapema leo akimkabidhi
mipira Katibu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Hollywood Riziki Senkonda,
Naibu Waziri Shonza ametoa vifaa mbalimbali vya michezo, Elimu na
Walemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 10,325,000 kwa Mkoa wa
Songwe.

Wachezaji wa Klabu ya Mpira wa
Miguu ya Hollywood wakifurahi baada ya kupokea jezi na mipira kutoka
kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana
Daniel Shonza mapema leo, Naibu Waziri Shonza ametoa vifaa mbalimbali
vya michezo, Elimu na Walemavu vyenye thamani ya shilingi milioni
10,325,000 kwa Mkoa wa Songwe.
*********************
Naibu Waziri
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Daniel Shonza
mapema leo ametoa vifaa mbalimbali vya michezo, Elimu na watu wenye
Ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 10,325,000 kwa Mkuu wa Mkoa
wa Songwe.
Naibu Waziri
Shonza ametoa Kompyuta Mbili, baiskeli mbili za watu wenye ulemavu,
mipira na jezi kwa Brig. Jen. Nicodemus Mwangela huku akimpongeza kwa
namna ambavyo amekuwa akiongoza jitihada mbalimbali za maendeleo ya Mkoa
wa Songwe.
“Nimeona nami
nije kuunga Mkono jitihada za Mkoa kama Naibu Waziri lakini pia mbunge
wa Mkoa wa Songwe, tunaziona Jitihada za Mkuu wa Mkoa katika kukuza
sekta mbalimbali, napenda kuwaambia huu ni mwanzo tu name nitaendelea
kuleta vitu mbalimbali.”, amesema Naibu Waziri Shonza.
Aidha ameupongeza
Uongozi wa Mkoa kwa kufanya maamuzi ya kununua timu ya Mpira wa Miguu
itakayocheza ligi kuu ambayo itaweza kuuwakilisha Mkoa wa Songwe kitaifa
na Kimataifa huku akiongeza kuwa Mkoa unafanya vizuri sana katika sekta
ya Michezo.
“Mara ya Kwanza
Mkoa wa Songwe kushiriki mashindano ya UMISETA ulishika namba moja
katika Mpira wa Miguu nchi nzima na mara ya pili ulishika nafasi ya
pili, hii ni ishara kuwa Songwe kuna vipaji vya kutosha.”, amesisitiza
Naibu Waziri Shonza
Naibu Waziri
Shonza amesisitiza kuwa jitihada hizi za kukuza sekta ya michezo
ziendane na kutafuta uwanja ambapo ameshauri uongozi wa Mkoa kuhakikisha
wanakuwa na uwanja wenye hati, uwe na uzio na usafishwe kisha maombi ya
kujengewa uwanja yawasilishwe Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini
(TFF).
Naye Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amempongeza Naibu Waziri Shonza
kwa kukumbuka nyumbani na kuleta vifaa hivyo ambavyo vimegusa sekta
Mbalimbali.
Brig. Jen.
Mwangela amesema wananchi wanaonyesha kupenda michezo hususani katika
kumiliki timu yao ya Mkoa hivyo wanaomba Wizara isaidie katika
upatikanaji wa haraka wa uwanja pale watakapo kamilisha taratibu za
awali zilizo elekezwa huku akiongeza kuwa vifaa alivyoleta vitaleta
matunda mazuri katika sekta za michezo na elimu.
Katibu wa CCM
Mkoa wa Songwe Mercy Mollel amempongeza Naibu Waziri Shonza kwa
Kukumbuka nyumbani kwao na kuleta vifaa hivyo ambavyo vitawafanya vijana
wajitume Zaidi hususani katika sekta ya michezo ili waweze kukumbukwa
na kuletewa vifaa vingine zaidi.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Mlowo Grace Kashililika amemshukuru Naibu Waziri Shonza kwa
kuipatia shule yake Kompyuta tano kwakuwa wamezoea kupewa ahadi na
wanasiasa lakini wamekuwa hawatimiziwi ahadi zao tofauti na yeye.
Kashililika
amesema sasa wataliomba Baraza la Mitihani Taifa ili mwakani wanafunzi
wa shule yake waweze kufanya mitihani ya kompyuta kwa vitendo kwakuwa
walishindwa kufanya hivyo kufuatia upungufu wa kompyuta.
Kwa upande wake
Nuru Mwasasu mama mzazi wa Mtoto mwenye ulemavu Mary Mwakanyamale
amemshukuru Naibu Waziri Sonza kwa kumpatia kiti kwa ajili ya mtoto wake
huyo mwenye ulemavu.
Amesema sasa
mtoto huyo mwenye umri wa miaka mtano lakini hawezi kukaa ataweza kukaa
kwa kutumia kiti hicho na kumpunguzia kulala muda wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...