Rais Mohamed Farmajo wa Somalia amekubali mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wa kukutana naye jijini Nairobi kwa ajili ya kutuliza hali ya mambo baada ya uhusiano wa pande mbili kuingia dosari hivi karibuni.
Rais wa Somalia amesema hayo baada ya kumpokea mjumbe maalumu wa Rais Kenyatta Bwana Fred Matiang’i Waziri wa Usalama wa Ndani aliyetumwa mjini Mogadishu kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo.
Rais wa Somalia amemhakikishia Matiang’i kwamba, atafanya safari hivi karibuni mjini Nairobi kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta ingawa hakutaja tarehe ya safari hiyo.
Uhusiano wa Kenya na Somalia uliingia dosari hivi karibuni baada ya wakazi wa Mandera kulazimishwa kutoroka makazi yao kufuatia ghasia zilizozuka kati ya wanajeshi wa Somalia dhidi ya wanajeshi wa eneo la Jubaland katika eneo la Bulla Hawa.
Baada ya tukio hilo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliionya serikali ya Somalia na kuitaka iache uchokozi wake wa mara kwa mara dhidi ya Kenya.
Rais Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa, “wanajeshi wa kigeni waliokiuka kanuni na kupuuza kabisa sheria za kimataifa na maazimio yaliyoafikiwa walitekeleza vitendo vya uchokozi na ukatili kwa kuwanyanyasa na kuharibu mali za raia wa Kenya wanaoishi katika mji wa mpakani wa Mandera”.
Kabla ya hapo pia, balozi na mwakilishi maalumu wa Somalia katika Umoja wa Mataifa alikuwa ameituhumu Kenya kwamba, inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kutishia kuishtaki serikali ya Nairobi katika umoja huo.
Matukio hayo yalionyesha ishara za kuvurugika uhusiano wa Kenya na Somalia hali iliyomfanya Rais Uhuru Kenyatta atume ujumbe maalumu katika nchi hiyo ya jirani kujaribu kutuliza mambo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...