Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akifungua jana kongamano la siku mbili la vijana katika fursa za
kilimo , mifugo na uvuvi ambao wameoka Tabora, Kigoma na Singida .

Vijana kutoka Tabora , Singida na
Kigoma wakiwa katika kongamano la siku mbili linalohusu fursa za kilimo
, mifugo na uvuvi. Kongamano hilo limefanyika jana mjini Tabora
NA TIGANYA VINCENT
VIJANA
wametakiwa kutumia fursa zinazotokana shughuli za kilimo na ufugaji
kujiari wenyewe badala ya kusubiri ajira za Serikali ili wawaze
kujiongezea kipato kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa
ujumla.
Kauli hiyo
imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua
kongamano la vijana katika fursa za kilimo , mifugo na uvuvi kwa
washiriki toka Tabora, Kigoma na Singida.
Alisema
Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imejitahidi kufikisha umeme vijijini
ambako ndiko mazao yanapatikana ili kuweza kuyaongezea thamani kwa
kuyasindika.
Mwanri alisema
hiyo ni fursa nzuri kwa vijana ya kutumia umeme ilikufanya kazi za
kuzalisha na kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi hivyo kuongeza
thamani na uhakika wa soko na bei nzuri.Alisema
uzalishaji wa mbegu bora za mazao nchini una uhitaji mkubwa na takwmi
zinaonyesha kuwa mahitaji ya mbegu ni tani 187,000 kwa mwaka wakati
uzalishaji wa ndani ni tani 71,000.
Mwanri aliongeza kuwa eneo hilo lina fursa kubwa kwa vijana kuzalisha mbegu kwani zinzhitajika kwa wingi.Alisema eneo
jingine ambalo ni fursa kwa vijana ni kilimo cha mazao ya mafuta ambapo
mahitaji ya mafuta ya kula ni lita 650,000 kwa mwaka wakati uwezo wa
nchi ni kuzalisha lita chini ya 250,000.
Mwanri alisema hali hiyo inatoa fursa kubwa kwa vijana kuzalisha mazao ya alizeti na michikichi.
Kwa upande wa
Mratibu wa Mkakati wa Taifa wa Vijana kushiriki katika Kilimo Revelian
Ngaiza alisema lengo kongamano hilo ni kutoa elimu kwa vijana nchini ili
waweze kushiriki katika uzalishaji mali kupitia kilimo na ufugaji ili
waweze kuinua kipato cha na Taifa kwa ujumla.
Alisema kauli
mbiu yetu ni “vijana,kilimo ni ajira” imelenga kuwasaidia vijana
kutambua na kufanya kilimo kuwa nguzo ya upatikanaji ajira nyingi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...